Baadhi ya watu wamefurahishwa na kile ambacho MSEVENI amepitisha kwamba anajenga maadili kwa kwa kutaza tabia ya ushoga kwa sheria kali,lakini tukumbuki kuwa watu wenye tabia ya ushoga ni binadam kama wewe,leo utasema vibaya kwa mashoga kwa kuwa ujui kama ndugu yako wa karibu mfano kama mtoto wako,baba yako,kaka yako mjomba wako na hata mdogo wako akawa na tabia hiyo,lakini leo unasema tuwatenge bila ya kujua ndugu zako ndo tabia yao.Binafsi si dhani kama itakuwa njia sahihi kuwanyanyasa mashoga eti kisa tabia zao,kumbuka shoga si mbaya ila tabia ya ushoga ndo ubaya wenyewe na tabia ukuwa na kusambaa,hivyo uliyefikiri kuwa kuwafunga mashoga ni sahihi basi umekosa nidhamu za haki ya binadam kwa kuwa wakosaji si mashoga tu bali hata wale wanao watumia mashoga kutimiza haja zao,KUWAFUNGA NA KUWANYANYASA SIO KUPUNGUZA MASHOGA.
kunahaja ya kuwa na SOMO LA MAADILI kwa watoto na hata vijana wa rika fulani,kuhusiana na mambo yote ambayo yanakuwa chukizo katika jamii.(MADAWA YA KULEVYA,UKIMWI,USHOGA,NA N.K)watu wajue namna yanavyopelekea mpaka kuingia katika mambo kama hayo na madhara hasa watoto wadogo ambao wanakuwa na hata vijana wanaokaribia kubarehe au wanao barehe.
kwa sababu tabia hizi chimbuko lake ni tangu utotoni.
Tuchukue hatua kabla ya tatizo kuwa kubwa.