Translate

Translate

Wednesday, 19 March 2014

DONA LA ZUA BALAA VIKOBA WALIVAMIA BUZA KWA MAMA KIBONGE,tazama picha



Ni hari isiyotegemewa na kila mtu katika mazingira yetu ,katika eneo moja lilipo BUZA maeneo ya kituo cha mama kibonge alimaarufu kama kwa dona limezua kasheshe baada ya eneo hilo kugawiwa kwa wananchi kwa ajili ya kufanya biashara ndogondogo,awali kabla maeneo haya jatolewa uongozi huo uliwatangazia watu kwa ajili ya kuandikisha majina na namba zao za simu ili waweze kuwagawia kwa utararatibu,wananchi zaidi ya 3000 waliitikia wito na kujiandikisha lakini baada ya muda kidogo utaratibu ukabadilika wakatangaza wanagawa maeneo bila kuita majina bali wanampatia mtu yeyote mwenye biashara hapo hapo jambo ili liliwakwaza baadhi ya watu walio andika majina.


Tathimini inaonyesha asilimia kubwa ya wafanya biashara hao ni wanachama mbalimbali wa VIKOBA baada ya kuwahoji asilimia kubwa ya watu walinithibitishia wao wapo katika VIKOBA .Tangu niingie vikoba sijawahi kuangaika kama jinsi nilivyokuwa katika mikopo ya saccos,benk na hata pride lakini sasa nina raha sana katika kikundi  kikoba hivyo lazima nijishughulishe ili nipate fedha ya marejesho ya hisa kila wiki,ni mama Faudhia alifunguka kwa furaha jinsi VIKOBA  inavyo mpa raha
Eneo ni kubwa linavyoonekana litahusisha michezo mbalimbali ya watoto mfano bembea,treni la umeme,na vitu vingi ambavyo wananchi walisikia kama fununu.
Mategemeo yetu eneo hili liwe kubwa kama Tandika sokoni ili nasi tuweze fanya biashara tujipatie kipato,tunamshukuru aliyejitolea kutupa maeneo kiukweli ameona mbali sana hatuna cha kumlipa ila Mungu ndo atamlipa.ni Aisha Mbeya mwanachama wa VIKOBA mkazi wa kata ya makangarawe aliongea maneno hayo kwa upole sana

Maeneo haya yanasemekana ni ya kanisa la Angrikana ,wanahabari wetu walijaribu kumtafuta kiongozi wa kanisa hakupatikana .

JE?KWA NINI SERIKALI NYINGI ZA MTAA HAZINA UBAO WA MATANGAZO KWA NJE?cheki picha katika blog

Tunapozungumzia serikali ya mtaa(local government)ni wazi kabisa wengi tunatambua tuna zungumzia serikali gani,kwa asilimia kubwa nchini serikali hii ipo kila mtaa kwa ajili ya wananchi wake na wala si kwa ajili ya viongozi wa serikalini lakini cha ajabu zaidi ni kwamba asilimia ya wananchi wengi wanaogopa kuwa karibu na serikali yao ambayo ipo kwa ajili yao wenyewe.
Mbao za matangazo aziwekwi kwa sababu ni sehemu ambayo wananchi ni rahisi kupata taarifa na kuhoji endapo taarifa sio sahii na mara nyingi taarifa zinakuwa na kasoro za kiubadhirifu.
Kuna vitu muhimu sana vya kuzingatia kama wananchi wa Tanzania hasa kwa ajili ya maendeleo yetu wenyewe kasumba kubwa ni kwamba tumenyimwa elimu ya kuelewa vitu vya msingi ili tuweze nyanyaswa pasipo na hatia,mara nyingi viongozi wa mtaa wakichaguliwa wanabadilika sana tunawanajiona tofauti na wananchi wa kawaida.
Sheria inatambua kabisa haki na wajibu wa mwananchi na viongozi,mwananchi anayo haki ya kuuliza na kuhoji swala la maendeleo katika mtaa wake pasipo kuvunja sheria ya nchi
KUMBUKA SERIKALI YA MTAA YOYOTE LAZIMA IWE NA UBAO WA MATANGAZO AMBAO UNAONYESHA MAPATO NA MATUMIZI NA TAARIFA ZINGINE MUHIMU.

Hivyo kama mwanajamii na haki yako kuuliza na kuhoji ni muhimu sana kufatilia ili kujiletea maendeleo sisi wenyewe lazima tuanze chini alafu ndo tupande juu.