Mwananchi ana
wajibu na majukumu yake kuhakikisha kuwa kiongozi aliyemchagua au kuteuliwa
anatimiza wajibu wake ipasavyo katika viwango vinavyokubalika katika eneo la
kijiji/mtaa kulingana na mipango na makibaliano ya vikao vya kisheria ya kijij
na mtaa.
Kila mwananchi
ana wajibu wa kupinga na kukataa kila aina ya uovu kayika jamii ikiwemo
rushwa,uonevu wizi ubadhilifu wa mali za umma nay a watu binafsi.
Wananchi pia
wana jukumu la kudai na kupigania haki zao na za wananchi wengine kutoa
malalamiko na kuuliza maswali juu ya mambo mbalimbali yananoendelea kijijini au
kwenye mtaa kupitia vyombo mbalimbali vya kijamii na kiserikali. Wananchi wanashiriki
katika serikali za mitaaa kupitia vikao au mikutano mbalimbali ambapo hujadili
na kutoa mapendekezo yao kuhusu mipango
na matatizo yanayowakabili kwa mamna moja au nyingine ili kuweza kupatiwa
ufumbuzi na kurahisisha uboreshaji wa huduma za kijamii katika maeneo yao
wanamoishi.