Translate

Translate

Thursday, 1 January 2015

JE? WAJUA WAJIBU WETU KWENYE SERIKALI ZA MTAA/KIJIJI? soma kwa utulivu utagundua mapungufu yetu na ya serikali usika

Mwananchi ana wajibu na majukumu yake kuhakikisha kuwa kiongozi aliyemchagua au kuteuliwa anatimiza wajibu wake ipasavyo katika viwango vinavyokubalika katika eneo la kijiji/mtaa kulingana na mipango na makibaliano ya vikao vya kisheria ya kijij na mtaa.
Kila mwananchi ana wajibu wa kupinga na kukataa kila aina ya uovu kayika jamii ikiwemo rushwa,uonevu wizi ubadhilifu wa mali za umma nay a watu binafsi.

Wananchi pia wana jukumu la kudai na kupigania haki zao na za wananchi wengine kutoa malalamiko na kuuliza maswali juu ya mambo mbalimbali yananoendelea kijijini au kwenye mtaa kupitia vyombo mbalimbali vya kijamii na kiserikali. Wananchi wanashiriki katika serikali za mitaaa kupitia vikao au mikutano mbalimbali ambapo hujadili na kutoa mapendekezo  yao kuhusu mipango na matatizo yanayowakabili kwa mamna moja au nyingine ili kuweza kupatiwa ufumbuzi na kurahisisha uboreshaji wa huduma za kijamii katika maeneo yao wanamoishi.

No comments: