Translate

Translate

Saturday, 12 April 2014

MIFUMO YA TATHIMINI NA UFATILIAJI WA RASILIMALI ZA UMMA(PETS)

Kuna aina kadhaa za mifumo ya tathmini ambayo inatumiwa kulingana na mahitaji au mazingira ya sehemu husika.mifumo hiyo ni kama vile;ufatiliaji wa Matumizi ya fedha za umma(public expenditure system and survey),ushirikishwaji wa jamii ya vijiji katika tathmini(participatory rural appraisal(PRA),tathmini ya uwajibikaji wa jamii(social accountability monitoring)na PIMA KADI
Mifumo yote hiyo imeainishwa utaratibu ambao unaweza kutumika katika kukusanya taarifa inayokusudiwa katika kuijenga jamii uwezo,kuiwezesha kuwa na kauli na kushiriki ipasavyo katika kutathimini na kuiwajibisha mamlaka husika pale inapobainika kuwa rasilimali za umma zimetumika  kinyume na jinsi ilivyokusudiwa.Mifumo yote hiyo ni sahihi na inafaa kutumika kilingana na chaguo la sehemu husika.
Katika muongozo huu ,mfumo mkuu wa tathmini utakaotumika na tutakaojikita nao zaidi ni mfumo wa ufatiliaji wa matumizi ya fedha za umma au PETS,pia tutaangalia kwa undani kuhusu zana ya PIMA KADI na jinsi inavyotumika kama nyenzo ya kukusanya taarifa.
Kwa ujumla PETS na mifumo yake imesaidia kujibu maswali ambayo mara nyingi wananchi wamekuwa wanajiuliza ili kupima tathimini ya fedha zilizopangwa au kutumika na matokeo husika .Hivyo kupitia PETS wananchi wanaweza kufanya tathimini na kupata ufumbuzi wa maswali yanayowakabili kuhusu mgawanyo wa matumizi ya rasilimali zao. Baadhi ya maswali ambayo wananchi hujiuliza ni kama yafuatayo
1)je,fedha na rasilimali za umma huwafikia wananchi hususani wale wa ngazi ya chini mfano wanawake na watoto kama ilivyokusudiwa ?
2)je,rasilimali fedha na rasilimali zingine zinawafikia wananchi kwenye maeneo husika kwa mtizamo wa kijinsia?
Utaona kuwa swali la kwanza linalohoji mtiririko wa fedha na rasilimali za umma zitolewazo ama na serikali kuu au wafadhili au wabia wa kimaendeleo ili kugharamia miradi ya maendeleo katika kijiji,kata.Mantiki yake ni kutaka kufahamu ni kiasi gani cha fedha na rasilimali za umma zimewafikia walengwa au watoa huduma,kama vile hospitali,shule ,maji ,barabara  nk kama ilivyokusudiwa.
Katika kufanya tathmini na kujiuliza maswali hayo ,na iwapo kuhoji huko kunaweza kukasababisha uchunguzi na ikadhihirika kuwepo na utofauti ya fedha zilizotolewa katika ngazi ya serikali kuu na kiasi kilichopelekwa kwa watoa huduma katika ngazi za nchini,huo unaitwa uvujaji.Hii inamaanisha kuwa baadhi ya pesa au rasilimali zilizotolewa kwa ajili ya miradi ya maendeleo,hazijatumika kulingana na sera au maleng yaliyokusudiwa na serikali au mamlaka husika.maana yake ni kuwa fedha au rasilimali hizi zimekwapuliwa katika ngazi Fulani ya kiutawala,inaweza kuwa wilayani au mikoani.
Hali kadhalika ,swali la pili linalenga zaidi katika uchambuzi.Lengo ni kubainisha kwa nini uvujaji hujitokeza.Mara nyingi,hujibu maswali kama vile ,kwa nini uvujaji hutokea katika baadhi ya halmashauri zaidi ya zingine?Au kwa nini shule ,halmashauri kadhaa hupokea fedha na rasilimali nyingi kuliko zingine
Kwa kufanya utambuzi huo ,mfumo unawezesha namna ya kufatilia ili kupunguza uvujaji na kuboresha utendaji na uwajibikaji katika ngazi ya ki-serikali /uongozi /utawala husika
Hivyo basi,ili kuondosha mianya ya rushwa na kuimarisha utawala bora katika ngazi zote husika za uongozi,ni vyema kutambua mianya ya rushwa,ambapo suala la kuwajengea uwezo wananchi au wapokeaji wa huduma,litaweza kusaidia usimamizi na udhibiti wa rasilimali katika maeneo yote.Pia kwa kutumia mfumo wa PETs wananchi watadai taarifa za matumizi kulingana na huduma zitolewazo ,pia watahoji kiwango cha utendaji kazi wanapokuwa na shaka ,hivyo kuzuia kushamiri kwa rushwa kwa viongozi wao.