Translate

Translate

Wednesday, 27 November 2013

MCHANGO WA DINI MBALIMBALI KATIKA KUTEKEKELAZAJI PETS

PETS kama dhana moja wapo wa ufatiliaji wa matumizi ya rasilimali za umma,inasukumwa na lengo kuu la kuona kuwa rasilimali za umma zinztumika ipasavyo na kwa mgao unaowiana ili kuleta maendeleo kwa makundi yote ya jamii.Mafnikio ya PETS kwa kiasi kikubwa yanategemea ushirikiano wa karibu baina ya vyombo , taasisi ,asasi,vikundi na makundi mbalimbali katika jamii ambapo yote kwa pamoja wanahusika katika kusimamia rasilimali za umma ili kuona maendeleo na ustawi wa jamii.

VIONGOZI WA DINI wananafasi kubwa sana katika masuala ya kiroho,pia dini zina wajibu mkubwa sana wa kuchangia katika masuala ya kawaida ya kibinadamu,hasa katika shughuli za ki- maendeleo na uchumi ili kuwasaidia waumini kukabiliana ba changamoto za maisha.DINI kama sehemu ya jamii ,zina wajibu na majukumu makubwa ya kushauri,kuelekeza,kuonya,kufundisha na kukemea mienendo yoyote isiyofaa na hasa inayokinzana na misingi yaUADILIFU,UWAJIBIKAJI,USAWA,na HAKI hivyo kuhamasisha waumini kumcha MUNGU ili kukomesha uharibifu na ubadhilifu na kusimamia vyema rasilimali za umma ili ziwe na faida kwa wote.
 MAENDELEO HAYANA DINI WALA KABIRA WOTE TUNAHATHIRIKA NA UBADHILIFU UNAO JITOKEZA HIVYO KWENYE MASUALA YA MAENDELEO WOTE WAMOJA.
   
ASANTE

JOSE MALI: JINSI JAMII INAVYOPOKEA VIZURI ELIMU YA PETS MKOAN...

JOSE MALI: JINSI JAMII INAVYOPOKEA VIZURI ELIMU YA PETS MKOAN...: wananchi wa karoleni moshi kilimanjaro wakitafakari  baada ya mafunzo ya PETS Baada ya vijana kutoka TAASISI mbalimbali ...

JINSI JAMII INAVYOPOKEA VIZURI ELIMU YA PETS MKOANI KILIMANJARO



wananchi wa karoleni moshi kilimanjaro
wakitafakari 
baada ya mafunzo ya PETS




Baada ya vijana kutoka TAASISI mbalimbali za dini kuweza kutoa elimu ya ufatiliaji wa matumizi wa rasilimali za umma, wananchi wamebaki wakitafakari kwa kina jinsi ya kufanya na wapi waanzie ili kujiridhisha na serikali yao.