Siku zote mazingira hutuzwa na watu
waliozunguuka mazingira hayo,ni wazi kabisa tunatambua mazingira ukiyatunza
nayo yanakutunza ila kinyume tutasema usipo ya tunza nao hayatakutunza.Yamkini
tunatambua fika umuhimu wa kutunza mazingira lakini tufanyapo jambo huku
tunajuwa ili nikosa maana yake tunakusudia kufanya kwa makusudi kabisa.
Kipindi cha mda mrefu sana wakaza wa buza walikuwa na kilio cha barabara ya rami yenye kurahisisha usafiri tena
ikawa kama ndo sababu ya watu kutumia kama sera katika kampeni zao za kujinadi
ya kwamba watatengeza barabara yenye kiwango lakini leo cha kushangaza wakazi hao wameonyesha dhahiri katika utunzaji wa mazingira ya barabara hiyo yenye kiwango cha rami.
Sehemu kubwa ya barabara watu
wanatupa takataka, hili jambo ni la kushangaza sana na nila aibu kama jamii kiujumla,mazingira ni
muhimu sana kuyatunza hasa katika sehemu ambazo tunaishi kila siku, pia
inakupasa kutambua mradi wowote unaotolewa na serikali kuhusiana na jamii yake
inakuhusu wewe na mwengine kwa sababu kile wanachopanga serikali ni mtazamo
kutoka katika jamii yake,kasumba yetu sisi watanzania ni kwamba kitu cha
chochote cha serikali tunakitumia hovyo bila kujisikia uchungu kumbe tunasahau
matokeo yale ni baada ya nguvu kazi zetu.
Jamani,haipendezi maneno kama haya
yawe yanaludiwa kwa kila siku yatachosha watu ila tutayaludia endapo watu
hawataonyesha ushirikiano lazima tuweke sheria ndogo ya kuzibiti uchafunzi wa
mazingira.Mwisho kabisa napenda kuwahasa viongozi wa serikali za mitaa kutafuta
maeneo maalumu ya kutupa takataka ili iwe rahisi kutunza mazingira yetu kwani
kutunza mazingira ni jambo muhimu sana hasa katika kutunza afya zetu kiujumla
lakini pia wananchi tuwe macho na kila mmoja awe mlinzi kwa mwenzie.