Translate

Translate

Friday, 2 January 2015

JE? TANZANIA INA UTAWALA BORA click usome kujua nini utawala bora

UTAWALA BORA
Utawala bora ni matumizi ya uwezo (mamlaka)wa kiserikali katika jitihada za kuongeza na kutumia rasilimali hizo ili kuboresha maisha ya wananchi
MISINGI YA UTAWALA BORA
v      Utawala wa kidemokrasia
v      Ushirikishwaji wa umma
v      Utawala wa kisheria
v      Haki na usawa kwa watu wote
v      Uwazi katika kuendesha shughuli za maendeleo
v      Uwajibikaji katika utendaji
v      Uadilifu
Misingi hii ikizingatiwa na kufanyiwa utekelezaji lazima mabadiliko yataonekana

Ili utawala bora uwe na sifa za kupendeza na kuendwa na wananchi lazima uzingatie Misingi ya utawala bora.

TEC MEDIA vs YOUTHCAN VIDEO

SOMA UFAHAMU KWA KINA JUU YA KAMATI ZA SERIKALI ZINAVYOKWENDA KINYUME NA SHERIA ZA NCHI kwa faida yetu sote

KAMATI  ZA HALMASHAURI YA KIJIJI/KAMATI YA MTAA

Ø Kuna kamati tatu za halmashauri ya kijiji/mtaa kisheria
Ø Kamati ya fedha,mipango na uchumi ,huduma za jamii na shughuli za kujitegemea na ulinzi na usalama
Ø Mkutano mkuu wa kijiji/mkutano wa wakazi wa mtaa una uwezo wa kuagiza halmashauri ya kijij/kamati ya mtaa kuundaa kamati ya muda kwa shughuli maalum au halmashauri yenyewe inaweza kuunda kukiwa na haja ya kufanya hivyo.
Ø Idadi ya wajumbe katika kamati inashauriwa wasipungue wajumbe watatu 3 na wasizidi wajumbe watano 5
Ø Kamati za kisheria inafaa ziongozwe na mjumbe wa halmashauri ya kijiji /kamati y mtaa
Ø Inashauriwa wenyekiti wa kijiji /mtaa , wenyeviti wa vitongoji  wasiwe wenyeviti wa kamati mbalimbali ili kutolimbikiza madaraka yote kwa halmashauri ya kijiji/kamati ya mtaa
Ø Wananchi  wakaida wanaweza kuwa wajumbe wa kamati au wanaweza kuitwa kutoa ushauri kwenye vikao vya kamati
Ø  Kamati zinaweza kukutana mara kwa mara kutunza kumbukumbu na kuendesha vikao kwa kushauriwa na afisa mtendaji wa kijiji (VEO)/ Afisa mtendaji wa mtaa(MEO)