KAMATI ZA HALMASHAURI YA KIJIJI/KAMATI YA MTAA
Ø Kuna kamati tatu za halmashauri ya
kijiji/mtaa kisheria
Ø Kamati ya fedha,mipango na uchumi
,huduma za jamii na shughuli za kujitegemea na ulinzi na usalama
Ø Mkutano mkuu wa kijiji/mkutano wa
wakazi wa mtaa una uwezo wa kuagiza halmashauri ya kijij/kamati ya mtaa kuundaa
kamati ya muda kwa shughuli maalum au halmashauri yenyewe inaweza kuunda kukiwa
na haja ya kufanya hivyo.
Ø Idadi ya wajumbe katika kamati
inashauriwa wasipungue wajumbe watatu 3 na wasizidi wajumbe watano 5
Ø Kamati za kisheria inafaa ziongozwe
na mjumbe wa halmashauri ya kijiji /kamati y mtaa
Ø Inashauriwa wenyekiti wa kijiji /mtaa
, wenyeviti wa vitongoji wasiwe
wenyeviti wa kamati mbalimbali ili kutolimbikiza madaraka yote kwa halmashauri
ya kijiji/kamati ya mtaa
Ø Wananchi wakaida wanaweza kuwa wajumbe wa kamati au
wanaweza kuitwa kutoa ushauri kwenye vikao vya kamati
Ø
Kamati
zinaweza kukutana mara kwa mara kutunza kumbukumbu na kuendesha vikao kwa
kushauriwa na afisa mtendaji wa kijiji (VEO)/ Afisa mtendaji wa mtaa(MEO)
No comments:
Post a Comment