Translate

Translate

Saturday, 26 April 2014

MKUKUTA NI NINI?soma ujilidhishe

MKUKUTA ni nini?NI kifupisho cha maneno ya Kiswahili yenye maana ya mkakati wa kukuza uchumi na kupunguza umasikini Tanzania.
MKUKUTA awamu ya 1(2005/06-2009/10)ulilenga katika kukuza uchumi ,kupunguza umasikini wa kipato ,ubora wa maisha ya watu na ustawi wa jamii pamoja na kuimarisha utawala bora na uwajibikaji .utekelezaji wake ulienda sambamba na uandaaji wa ripoti za kila mwaka zikiainisha uzoefu ,mafanikio na changamoto.
Kila mwaka ripoti zilijadiliwa na wadau mbalimbali katika makongamano na mikutano ya kitaifa ya sera.Maoni kutoka kwenye mapitio na mijadala hiyo yalitumika katika kuboresha mpango wa mwaka uliofuata.
MKUKUTA inachangia katika utekelezaji wa dira ya taifa ya maendeleo(2025)na malengo ya maendeleo ya millennia (2015).