MKUKUTA ni nini?NI kifupisho cha maneno ya Kiswahili yenye maana ya
mkakati wa kukuza uchumi na kupunguza umasikini Tanzania.
MKUKUTA awamu ya 1(2005/06-2009/10)ulilenga katika kukuza uchumi
,kupunguza umasikini wa kipato ,ubora wa maisha ya watu na ustawi wa jamii
pamoja na kuimarisha utawala bora na uwajibikaji .utekelezaji wake ulienda
sambamba na uandaaji wa ripoti za kila mwaka zikiainisha uzoefu ,mafanikio na
changamoto.
Kila mwaka ripoti zilijadiliwa na wadau mbalimbali katika makongamano na
mikutano ya kitaifa ya sera.Maoni kutoka kwenye mapitio na mijadala hiyo
yalitumika katika kuboresha mpango wa mwaka uliofuata.
MKUKUTA inachangia katika utekelezaji wa dira ya taifa ya
maendeleo(2025)na malengo ya maendeleo ya millennia (2015).
No comments:
Post a Comment