Translate

Translate

Tuesday, 6 January 2015

MALENGO YA UFUATILIAJI- PETS

PETS imethibitika kuwa ni kati ya zana na nyenzo muhimu katika ufuatiliaji wa matumizi ya rasilimali za umma , hasa pale inapofanyika kwa mitizamo wa kijinsia . Hivyo basi , PETS inalenga kufanikisha yafuatayo;

Ø Kuboresha utoaji huduma ; kufuatilia matumizi ya fedha au rasilimali za umma kwa mtizamo wa kijinsia , kunasaidia sana kuchochea uboreshaji wa utoaji wa huduma mbalimbali za kijamii kwa ubora uliokusudiwa . vile vile kuhakikisha kuwa rasilimali zimeenda kutekeleza lengo kusudiwa na kuhakiki thamani halisi ya fedha zilizotumika.
Ø Kuhakiki utendaji wa serikali na mamlaka husika; mfumo huu unasaidia sana katika kuhakiki utendaji wa serikali na mamlaka husika ,hasa katika ngazi za vitongoji na vijiji au katika vikundi vidogo vidogo , kwa kusoma nyaraka , ripoti na taarifa mbalimbali za utekelezaji.
Ø Kukuza uwajibikaji;  Hii inaanzia kwa wananchi kwa maana ya wanawake , wanaume , vijana , walemavu na makundi mengine yaliyoko pembezoni , ambapo hushiriki moja kwa moja katika kuhoji serikali .sanjali na hilo huhakikisha kwamba viongozi wanatenda kila ambacho wanapaswa kutenda kulingana na mipango.
Ø Kuwezesha uandaaji wa mipango shirikishi ya maendeleo;  Taarifa zinawafanya wananchi waweze kushiriki vizuri katika uandaaji wa mipango ,au katika kubaini aina ya miradi itakayotekelezwa kwenye jamii hisika