PETS imethibitika kuwa ni kati ya zana na
nyenzo muhimu katika ufuatiliaji wa matumizi ya rasilimali za umma , hasa pale
inapofanyika kwa mitizamo wa kijinsia . Hivyo basi , PETS inalenga kufanikisha
yafuatayo;
Ø Kuboresha utoaji huduma ; kufuatilia matumizi ya fedha au rasilimali za umma kwa
mtizamo wa kijinsia , kunasaidia sana kuchochea uboreshaji wa utoaji wa huduma
mbalimbali za kijamii kwa ubora uliokusudiwa . vile vile kuhakikisha kuwa
rasilimali zimeenda kutekeleza lengo kusudiwa na kuhakiki thamani halisi ya
fedha zilizotumika.
Ø Kuhakiki utendaji wa serikali na mamlaka husika; mfumo huu unasaidia sana katika
kuhakiki utendaji wa serikali na mamlaka husika ,hasa katika ngazi za vitongoji
na vijiji au katika vikundi vidogo vidogo , kwa kusoma nyaraka , ripoti na
taarifa mbalimbali za utekelezaji.
Ø Kukuza uwajibikaji; Hii inaanzia kwa wananchi kwa
maana ya wanawake , wanaume , vijana , walemavu na makundi mengine yaliyoko
pembezoni , ambapo hushiriki moja kwa moja katika kuhoji serikali .sanjali na
hilo huhakikisha kwamba viongozi wanatenda kila ambacho wanapaswa kutenda
kulingana na mipango.
Ø Kuwezesha uandaaji wa mipango shirikishi ya maendeleo; Taarifa zinawafanya wananchi waweze kushiriki
vizuri katika uandaaji wa mipango ,au katika kubaini aina ya miradi
itakayotekelezwa kwenye jamii hisika
No comments:
Post a Comment