HAKI ZA UHALALI WA MWANANCHI KUFATILIA MATUMIZI YA RASILIMALI ZA
UMMA(PETS)
Haki ni stahili ya binadam .Hii inamaanisha kuwa mtu ana haki kwa kuwa
anastahili ya kutenda jambo Fulani,au wengine wanatakiwa kutenda au kumtendea
jambo Fulani katika hali Fulani . Haki zinaweza kuwa binafsi au za jumla . Kwa
lugha rahisi ,tunasema kuwa haki ni stahili za msingi ambazo binadamu yeyote Yule
bila kujali jinsia ,umri ,itikadi,dini,rangi ,kabila au aina yoyote ya utofauti
huzaliwa nazo na hazitolewi na mtu na wala haziwezi kuondolewa na mtu kwa
sababu yeyote .vivyo hivyo ,uhalali wa mtu kufanyanya au kufanyiwa jambo Fulani
,unatikana na stahili ambayo mtu au wattu wanakuwa nayo kw mujibu wa sheria
,sera kanuni ,taratibu au muongozo husika,Ni kwa muktadha huo,wananchi kupitia
sheria ,sera,matamko ,mikataba ,kanunui na miongozo mbalimbali ,wanapata haki
na uhalali wa kufuatilia matumizi ya rasilimali za umma kila mara wanapoona
inafaa kufanya hivyo
NB;VYANZO VYA
HAKI
a)mila na desturi
b)katiba ya nchi
c)sera na miongozo
c)sheria za nchi
d)kanuni na mikataba ya kitaifa /kimataifa