Translate

Translate

Tuesday, 18 March 2014

TAKATAKA KANDO YA BARABARA UCHAFUNZI WA MAZINGIRA




Siku zote mazingira hutuzwa na watu waliozunguuka mazingira hayo,ni wazi kabisa tunatambua mazingira ukiyatunza nayo yanakutunza ila kinyume tutasema usipo ya tunza nao hayatakutunza.Yamkini tunatambua fika umuhimu wa kutunza mazingira lakini tufanyapo jambo huku tunajuwa ili nikosa maana yake tunakusudia kufanya kwa makusudi kabisa.
Kipindi cha mda mrefu sana wakaza wa buza walikuwa na kilio cha barabara ya rami yenye kurahisisha usafiri tena ikawa kama ndo sababu ya watu kutumia kama sera katika kampeni zao za kujinadi ya kwamba watatengeza barabara yenye kiwango lakini leo cha kushangaza wakazi hao wameonyesha dhahiri katika utunzaji wa mazingira ya barabara hiyo yenye kiwango cha rami.
Sehemu kubwa ya barabara watu wanatupa takataka, hili jambo ni la kushangaza sana  na nila aibu kama jamii kiujumla,mazingira ni muhimu sana kuyatunza hasa katika sehemu ambazo tunaishi kila siku, pia inakupasa kutambua mradi wowote unaotolewa na serikali kuhusiana na jamii yake inakuhusu wewe na mwengine kwa sababu kile wanachopanga serikali ni mtazamo kutoka katika jamii yake,kasumba yetu sisi watanzania ni kwamba kitu cha chochote cha serikali tunakitumia hovyo bila kujisikia uchungu kumbe tunasahau matokeo yale ni baada ya nguvu kazi zetu.

Jamani,haipendezi maneno kama haya yawe yanaludiwa kwa kila siku yatachosha watu ila tutayaludia endapo watu hawataonyesha ushirikiano lazima tuweke sheria ndogo ya kuzibiti uchafunzi wa mazingira.Mwisho kabisa napenda kuwahasa viongozi wa serikali za mitaa kutafuta maeneo maalumu ya kutupa takataka ili iwe rahisi kutunza mazingira yetu kwani kutunza mazingira ni jambo muhimu sana hasa katika kutunza afya zetu kiujumla lakini pia wananchi tuwe macho na kila mmoja awe mlinzi kwa mwenzie.

No comments: