Tunapozungumzia serikali ya mtaa(local government)ni wazi kabisa wengi
tunatambua tuna zungumzia serikali gani,kwa asilimia kubwa nchini serikali hii
ipo kila mtaa kwa ajili ya wananchi wake na wala si kwa ajili ya viongozi wa
serikalini lakini cha ajabu zaidi ni kwamba asilimia ya wananchi wengi
wanaogopa kuwa karibu na serikali yao ambayo ipo kwa ajili yao wenyewe.
Mbao za matangazo aziwekwi kwa sababu ni sehemu ambayo wananchi ni
rahisi kupata taarifa na kuhoji endapo taarifa sio sahii na mara nyingi taarifa
zinakuwa na kasoro za kiubadhirifu.
Kuna vitu muhimu sana vya kuzingatia kama wananchi wa Tanzania hasa kwa
ajili ya maendeleo yetu wenyewe kasumba kubwa ni kwamba tumenyimwa elimu ya
kuelewa vitu vya msingi ili tuweze nyanyaswa pasipo na hatia,mara nyingi
viongozi wa mtaa wakichaguliwa wanabadilika sana tunawanajiona tofauti na
wananchi wa kawaida.
Sheria inatambua kabisa haki na wajibu wa mwananchi na
viongozi,mwananchi anayo haki ya kuuliza na kuhoji swala la maendeleo katika
mtaa wake pasipo kuvunja sheria ya nchi
KUMBUKA SERIKALI YA MTAA YOYOTE LAZIMA IWE NA UBAO WA MATANGAZO AMBAO
UNAONYESHA MAPATO NA MATUMIZI NA TAARIFA ZINGINE MUHIMU.
Hivyo kama mwanajamii na haki yako kuuliza na kuhoji ni muhimu sana
kufatilia ili kujiletea maendeleo sisi wenyewe lazima tuanze chini alafu ndo
tupande juu.
No comments:
Post a Comment