Translate

Translate

Wednesday, 30 October 2013

TANZANIA HATUNA VIONGOZI WAADILIFU.

Hisia zangu zinanituma kuandika maneno haya.
Ni wazi kabisa viongozi hapa nchini hawajui nini maana ya uadilifu au kama kama wanajua basi wanakusudia kufanya mambo yasiofaa katika jamii,sina maana ya viongozi wote si waadilifu ila penye asilimia nyingi basi tutasema karibia wote,waliokuwa waadilifu basi hawana nguvu ya kusema wala si raisi kujionyesha,UADILIFU ni neno pana sana na linaweza likawa soma kubwa sana ambalo viongozi wetu walitakiwa kupatiwa kabla hawajaanza kupokea madaraka kimsingi UADILIFU inajumuisha tabia zote ambazo zinampendeza binadamu katika kutenda haki na kumjali na kumuhurumia zaidi ya kujiurumia wewe mwenyewe,UADILIFU ni kufanya jambu zaidi bila kujali maslahi yako na ikiwezekana kuongeza zaidi ya uwezo wa kawaida ambao mtu si raisi kujitoa dhana hii inabeba tabia nyingi mfano lazima uwe na HEKIMA,BUSARA,UPOLE,UTARATIBU,MWENYE SIFA YA PEKEE,UPENDO,UKWELI,MWAJIBIKAJI KULIKO KAWAIDA,HURUMA na n.k hizi zote ni UADILIFU tunamifano ya watu duniani waliokuwa waadilifu kihistoria YESU CHRISTU,MTUME MOHAMAD na n.k,UADILIFU ni ile hari ya kujitolea kufanya jambo kwa ajili ya mtu mwingine bila kujali kitakacho kukuta ili kumpendeza MUNGU wako kulingana na imani.
Binafsi ningewaasa viongozi wa TANZANIA kujifunza UADILIFU ili kuweza kuifikisha mbali nchi yetu wajue kuurumia watoto,wamama,wazee,wa baba,vijana na hata walemavu ili siku moja wapate neema ya MUNGU.
                                asante.

No comments: