Makala
leo asubuhi nikiwa katika safari zangu nimekerwa sana na hili la mbagala bus terminal nadhani hata wewe kama mwananchi wa mbagala unalijua hilo na linakukela pia
kwa wale ndugu zangu mliofika mbagala bus terminal mnajua hali halisi katika stand hiyo ya mabasi makubwa na madogo , ni wazi kabisa serikali inatambua kama ni wajibu wao katika uboreshaji , lakini tunasema uwajibikaji na utawala bora ni kasumba nzito sana nchi
katika kuuliza uliza kwangu inasemekana kila basi linaloingia pale linalipa ushuru kwa ajili ya stand bila shaka hata wafanyabiashara pale wanalipa ushuru wa eneo la stand yamkini hata wewe ni mmoja wapo katika sehemu fulani unalipa kodi au ushuru wa serikali , lakini kama wananchi tunahaki ya kujua fedha hizo tunazo katwa ni kwa ajili ya matumizi yapi. Mbagala inatambulika kila sehemu nje na ndani ya nchi kibiashara na hata kimapato ya nchi
kwenu wahusika wakuu katika uboreshaji wa mazingira ya mbagala bus terminal ni wazi mnapata mapato yetu lakini hamtaki kuyafanyia kazi iweje terminal kubwa kama mbagala bado inavumbi chini mpangilio mbovu wa magari hata mazingira ya usafi hakuna uduma za choo hazilidhishi?
Watanzania wenzangu bila kusimama wenyewe hatuta weza kusimamishwa sisi ndo watu wa kufanya mabadiko tuachane na mambo ya umimi tuungane kuweza kujiwekea mazingira salama wenyewe kwani uwezi mkuta mtoto wa viongozi wa kiwa katika mazingara ambayo tunayaishi sisi.
Tusisubiri kusukumwa tuanze wenyewe.
No comments:
Post a Comment