Translate

Translate

Friday, 21 March 2014

KAULI YENU IWE TANZANIA KWANZA maneno ya DR KIKWETE KWA BUNGE MAALUMU

Baada ya kuzungumza maneno ya yakufuraisha na kujenga bungeni RAIS DR Jakay Mrisho kikwete
ni wazi kabisa alionyesha hisia jinsi anavyoipenda nchi yake baada ya kuzungumza kwa kirefu sana
 aliwaasa wabunge kuwa kauli mbiu ya kusema TANZANIA KWANZA

GARI LA ANOTHER G YAPATA AJARI UKO MKOANI NJOMBE fungua utazame picha ya ajari mbaya

 kampuni ya another G iliyopo mkoani njombe yapata pigo baada ya gari moja kupata ajari mbaya

LIVE BUNGENI RAIS DR JAKAYA MRISHO KIKWETE AKIZUNGUMZIA JUU YA SERIKARI TATU


Wednesday, 19 March 2014

DONA LA ZUA BALAA VIKOBA WALIVAMIA BUZA KWA MAMA KIBONGE,tazama picha



Ni hari isiyotegemewa na kila mtu katika mazingira yetu ,katika eneo moja lilipo BUZA maeneo ya kituo cha mama kibonge alimaarufu kama kwa dona limezua kasheshe baada ya eneo hilo kugawiwa kwa wananchi kwa ajili ya kufanya biashara ndogondogo,awali kabla maeneo haya jatolewa uongozi huo uliwatangazia watu kwa ajili ya kuandikisha majina na namba zao za simu ili waweze kuwagawia kwa utararatibu,wananchi zaidi ya 3000 waliitikia wito na kujiandikisha lakini baada ya muda kidogo utaratibu ukabadilika wakatangaza wanagawa maeneo bila kuita majina bali wanampatia mtu yeyote mwenye biashara hapo hapo jambo ili liliwakwaza baadhi ya watu walio andika majina.


Tathimini inaonyesha asilimia kubwa ya wafanya biashara hao ni wanachama mbalimbali wa VIKOBA baada ya kuwahoji asilimia kubwa ya watu walinithibitishia wao wapo katika VIKOBA .Tangu niingie vikoba sijawahi kuangaika kama jinsi nilivyokuwa katika mikopo ya saccos,benk na hata pride lakini sasa nina raha sana katika kikundi  kikoba hivyo lazima nijishughulishe ili nipate fedha ya marejesho ya hisa kila wiki,ni mama Faudhia alifunguka kwa furaha jinsi VIKOBA  inavyo mpa raha
Eneo ni kubwa linavyoonekana litahusisha michezo mbalimbali ya watoto mfano bembea,treni la umeme,na vitu vingi ambavyo wananchi walisikia kama fununu.
Mategemeo yetu eneo hili liwe kubwa kama Tandika sokoni ili nasi tuweze fanya biashara tujipatie kipato,tunamshukuru aliyejitolea kutupa maeneo kiukweli ameona mbali sana hatuna cha kumlipa ila Mungu ndo atamlipa.ni Aisha Mbeya mwanachama wa VIKOBA mkazi wa kata ya makangarawe aliongea maneno hayo kwa upole sana

Maeneo haya yanasemekana ni ya kanisa la Angrikana ,wanahabari wetu walijaribu kumtafuta kiongozi wa kanisa hakupatikana .

JE?KWA NINI SERIKALI NYINGI ZA MTAA HAZINA UBAO WA MATANGAZO KWA NJE?cheki picha katika blog

Tunapozungumzia serikali ya mtaa(local government)ni wazi kabisa wengi tunatambua tuna zungumzia serikali gani,kwa asilimia kubwa nchini serikali hii ipo kila mtaa kwa ajili ya wananchi wake na wala si kwa ajili ya viongozi wa serikalini lakini cha ajabu zaidi ni kwamba asilimia ya wananchi wengi wanaogopa kuwa karibu na serikali yao ambayo ipo kwa ajili yao wenyewe.
Mbao za matangazo aziwekwi kwa sababu ni sehemu ambayo wananchi ni rahisi kupata taarifa na kuhoji endapo taarifa sio sahii na mara nyingi taarifa zinakuwa na kasoro za kiubadhirifu.
Kuna vitu muhimu sana vya kuzingatia kama wananchi wa Tanzania hasa kwa ajili ya maendeleo yetu wenyewe kasumba kubwa ni kwamba tumenyimwa elimu ya kuelewa vitu vya msingi ili tuweze nyanyaswa pasipo na hatia,mara nyingi viongozi wa mtaa wakichaguliwa wanabadilika sana tunawanajiona tofauti na wananchi wa kawaida.
Sheria inatambua kabisa haki na wajibu wa mwananchi na viongozi,mwananchi anayo haki ya kuuliza na kuhoji swala la maendeleo katika mtaa wake pasipo kuvunja sheria ya nchi
KUMBUKA SERIKALI YA MTAA YOYOTE LAZIMA IWE NA UBAO WA MATANGAZO AMBAO UNAONYESHA MAPATO NA MATUMIZI NA TAARIFA ZINGINE MUHIMU.

Hivyo kama mwanajamii na haki yako kuuliza na kuhoji ni muhimu sana kufatilia ili kujiletea maendeleo sisi wenyewe lazima tuanze chini alafu ndo tupande juu.

Tuesday, 18 March 2014

TAKATAKA KANDO YA BARABARA UCHAFUNZI WA MAZINGIRA




Siku zote mazingira hutuzwa na watu waliozunguuka mazingira hayo,ni wazi kabisa tunatambua mazingira ukiyatunza nayo yanakutunza ila kinyume tutasema usipo ya tunza nao hayatakutunza.Yamkini tunatambua fika umuhimu wa kutunza mazingira lakini tufanyapo jambo huku tunajuwa ili nikosa maana yake tunakusudia kufanya kwa makusudi kabisa.
Kipindi cha mda mrefu sana wakaza wa buza walikuwa na kilio cha barabara ya rami yenye kurahisisha usafiri tena ikawa kama ndo sababu ya watu kutumia kama sera katika kampeni zao za kujinadi ya kwamba watatengeza barabara yenye kiwango lakini leo cha kushangaza wakazi hao wameonyesha dhahiri katika utunzaji wa mazingira ya barabara hiyo yenye kiwango cha rami.
Sehemu kubwa ya barabara watu wanatupa takataka, hili jambo ni la kushangaza sana  na nila aibu kama jamii kiujumla,mazingira ni muhimu sana kuyatunza hasa katika sehemu ambazo tunaishi kila siku, pia inakupasa kutambua mradi wowote unaotolewa na serikali kuhusiana na jamii yake inakuhusu wewe na mwengine kwa sababu kile wanachopanga serikali ni mtazamo kutoka katika jamii yake,kasumba yetu sisi watanzania ni kwamba kitu cha chochote cha serikali tunakitumia hovyo bila kujisikia uchungu kumbe tunasahau matokeo yale ni baada ya nguvu kazi zetu.

Jamani,haipendezi maneno kama haya yawe yanaludiwa kwa kila siku yatachosha watu ila tutayaludia endapo watu hawataonyesha ushirikiano lazima tuweke sheria ndogo ya kuzibiti uchafunzi wa mazingira.Mwisho kabisa napenda kuwahasa viongozi wa serikali za mitaa kutafuta maeneo maalumu ya kutupa takataka ili iwe rahisi kutunza mazingira yetu kwani kutunza mazingira ni jambo muhimu sana hasa katika kutunza afya zetu kiujumla lakini pia wananchi tuwe macho na kila mmoja awe mlinzi kwa mwenzie.

Monday, 3 March 2014

KUWAFUNGA NA KUWANYANYASA SIO NJIA SAHIHI YA KUPUNGUZA USHOGA

Inawezekana ikawa ni furaha kwako kwakuwa upendi tabia ya ushoga ingawa unapenda kuzini,wengi wanasema kwamba dhambi kubwa sana kuwa shoga maana yake shoga awezi kuingia mbinguni ni wazi kabisa tofauti na mawazo ya MUNGU.Na sowezi amini kwamba mungu anaweza mchukia mtu sababu ya tabia yake.
Baadhi ya watu wamefurahishwa na kile ambacho MSEVENI amepitisha kwamba anajenga maadili kwa kwa kutaza tabia ya ushoga kwa sheria  kali,lakini tukumbuki kuwa watu wenye tabia ya ushoga ni binadam kama wewe,leo utasema vibaya kwa mashoga kwa kuwa ujui kama ndugu yako wa karibu mfano kama mtoto wako,baba yako,kaka yako mjomba wako na hata mdogo wako akawa na tabia hiyo,lakini leo unasema tuwatenge bila ya kujua ndugu zako ndo tabia yao.Binafsi si dhani kama itakuwa njia sahihi kuwanyanyasa mashoga eti kisa tabia zao,kumbuka shoga si mbaya ila tabia ya ushoga ndo ubaya wenyewe na tabia ukuwa na kusambaa,hivyo uliyefikiri kuwa kuwafunga mashoga ni sahihi basi umekosa nidhamu za haki ya binadam kwa kuwa wakosaji si mashoga tu bali hata wale wanao watumia mashoga kutimiza haja zao,KUWAFUNGA NA KUWANYANYASA SIO KUPUNGUZA MASHOGA.
kunahaja ya kuwa na SOMO LA MAADILI kwa watoto na hata vijana wa rika fulani,kuhusiana na mambo yote ambayo yanakuwa chukizo katika jamii.(MADAWA YA KULEVYA,UKIMWI,USHOGA,NA N.K)watu wajue namna yanavyopelekea mpaka kuingia katika mambo kama hayo na madhara hasa watoto wadogo ambao wanakuwa na hata vijana wanaokaribia kubarehe au wanao barehe.
kwa sababu tabia hizi chimbuko lake ni tangu utotoni.
Tuchukue hatua kabla ya tatizo kuwa kubwa.