Translate

Translate

Friday, 4 April 2014

SOMA KWA MAKINI UTANGULIZI HUU WA RASIMU YA JAMHURI TA MUUNGANO WA TAZANIA

Kwa kuwa, sisi wananchi wa jamhuri wa muungano wa Tanzania tumeamua rasmi na kwa dhati kujenga katika nchi yetu jamii inayoheshimu na kuzingatia misingi ya utu,uhuru,haki,usawa,udugu,amani,umoja na mshikamano katika Nyanja zote za maisha yetu;


Na kwa kuwa,tunaamini kuwa misingi hiyo inaweza tu kutekelezwa katika jamii yenye mfumo wa kidemokrasia na utawala bora ambayo serikali yake inasimamiwa na Bunge lenye Wabunge waliochaguliwa na wanaowakilisha wananchi,na Mahakama huru zinazotekeleza wajibu wa kutoa haki bila woga wala upendeleo kudumisha na kwamba wajibu wa kila mtu unatekelezwa kwa uaminifu
Na kwakuwa ,tunatambua umuhimu wa kutunza mali ya mamlaka ya nchi na pamoja,kupiga vita aina zote za uharibifu,ubadhirifu na kuhimiza matumizi bora na endelevu ya rasilimali na mustakabali wa maisha ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo;
Na kwa kuwa,tunatambua umuhimu na faida za kujenga,kukuza na kuendeleza amani,umoja,urafiki na ushirikianao  miungoni mwa watanzania,mataifa mbalimbali ya Afrika na duniani kwa ujumla;
Na kwa kuwa,azma ya kujenga umoja wa bara la Afrika inadhihirishwa na Muungano wa iliyokuwa jamhuri ya Tanganyika na jamhuri ya watu Zanzibar;
Na  kwa kuendeleza dhamira yetu hiyo,ni muhimu:
a)kulinda,kuimarisha na kuudumisha muungano wa  nch za jamhuri ya Tanganyika na jamhuri ya watu wa Zanzibar;
b)kujenga Taifa huru na linalojitegemea;
c)kuimarisha na kuendeleza utawala wa sheria;
d)kukuza na kuendeleza maadili,uwajibikaji na uwazi;
e)kujenga umoja na mshikamano utakaowezesha kutimiza malengo ya kisiasa,kiuchumi ,kijamii,kimazingira na kulinda urithi kwa ujumla;
f)kujenga na kuendeleza ukuu wa mamlaka ya watu;
g)kujenga na kuendeleza utii wa mamlaka ya katiba;na
h)kuimarisha na kudumisha uzalendo kwa taifa miungoni mwa watanzania;
NA KWA KUZINGATIA,urithi tulioachiwa wa waasisi wa Taifa letu wa kujenga nchi yenye umoja wa watu wake ambao hawabaguani kwa misingi ya ukabila,dini ,rangi,jinsi au ubaguzi wa aina nyingine yoyote;
NA KUZINGATIA,uzoefu wa zaidi ya miaka hamsini ya uhuru wa Tanganyika,miaka hamsini ya mapinduzi ya Zanzibar na miaka hamsini ya muungano wa jamhuri ya Tanganyika na jamhuri ya watu wa Zanzibar,na uhumuhimu wa ushiriki mpana na bayana wa wananchi katika utungaji wa katiba ya jamhuri  ya muungano wa Tanzania;
HIVYO BASI,KATIBA HII YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA ILIYOPENDEKEZWA NA BUNGE MAALUM LA KATIBA imetungwa na SISI WANACHI WA JAMHURI YA MUUNGANO WATANZANIA kupitia KURA YA MAONI kwa madhumuni ya kujenga jamii kama hiyo,na kuhakikisha kuwa jamhuri ya muungano wa Tanzania inaongozwa na serikali yenye kufuata misingi ya demokrasia na utawala wa sheria,kujitegemea na isiyofungamana na dini.



 TOA MAONI YAKO

No comments: