Tatizo la
Maji safi Mtaa wa Makangarawe, katika Kata ya Makangarawe Wilaya ya Temeke jiji
Dar es salaam umezidi kuwa ni shida kwa wananchi, jambo ambalo linapelekea
wananchi wengi kutumia visima vya watu binafsi ambavyo usalama wa maji si mzuri
kiafya .
Akizungumza
kwenye mkutano wa wananchi mwenyekiti wa sasa Ndugu Juma Mohamed Kibanda juu ya
tatizo la mradi huo kufika huko alisema”hii inatokana na usimamizi mbovu wa
uongozi uliopita madarakani ,uongozi kukosa uwazi na uwajibikaji jambo ambalo
limepelekea mradi huu wa maji safi na salama kufa na wananchi wetu kuangaika”
Baadhi ya
mfumo wa mabomba ya maji yamepasuka kusabisha maji mengi kuvuja na kusambaa
maeneo mbalimbali ya mtaa, na kusababisha uchafuzi wa mazingira katika maeneo
hayo ambapo ni hatari kwa afya ya jamii iliyo zunguka maeneo hayo.
Uongozi
utambue wananchi wako katika mazingira hatarishi ya kiafya na hata upatikanaji
wa maji safi na salama hivyo iwe ni changamoto kwao ili kutafuta ufumbuzi wa
tija kuondoa tabu hiyo.
Na; Joseph
malisa