Translate

Translate

Wednesday, 11 February 2015

TASAF MTAA WA MAKANGARAWE TEMEKE WAZUA MASWALI MENGI

TASAF MTAA WA MAKANGARAWE TEMEKE WAZUA MASWALI MENGI
Mpango wa serikali wa kunusuru kaya maskini awamu ya tatu (TASAF) ukiwa katika utekelezaji wake wa kuhakikisha wanawafikia walengwa wa mradi huo ambao kaya maskini umepelekea kuwemo kwa maswali mengi ya msingi  kutoka kwa baadhi ya wananchi walio hudhuria kikao hicho mtaa Makangarawe,Kata ya Makangarawe, Wilaya Temeke Dar es salaam.



Akizungumza katika mkutano   mwenyekiti wa mtaa Juma Mohamed Kibanda alisema"Mpango huu wa TASAF ni mpango wa kunusuru kaya maskini ambao kwa sasa umetufika wanamakangarawe hivyo tushirikiane katika kufikia lengo na kuwafikia walengwa"aliendelea kusema "Mpango huu ni wamendeleo hasa katika kaya maskini ". Akizungumza  mwezeshaji wa TASAF ambae alielezea malengo na faida za mpango huo wa TASAF. Jambo ambalo lilizua maswali mengi na hoja za msingi kutoka kwa wanajamii wa Makangarawe  ili kujilidhisha kama mpango huo ni waukweli au ni jambo la kisiasa ambalo linaleta mkanganyiko kutokana na ukaribu wa uchaguzi jambo ambalo lishawahi kujitokeza mwaka 2005 .
Kufatiwa mkutano huo mwenyekiti Juma Kibanda aliwasihi hasa vijana wajitambue na waitambue serikali yao hasa katika maswala ya kimaendeleo na kuleta mabadiliko katika mtaa wao.


No comments: