Translate

Translate

Friday, 13 February 2015

MRADI WA MAJI SAFI MAKANGARAWE NI TATIZO KWA WANANCHI

Tatizo la Maji safi Mtaa wa Makangarawe, katika Kata ya Makangarawe Wilaya ya Temeke jiji Dar es salaam umezidi kuwa ni shida kwa wananchi, jambo ambalo linapelekea wananchi wengi kutumia visima vya watu binafsi ambavyo usalama wa maji si mzuri kiafya .


Akizungumza kwenye mkutano wa wananchi mwenyekiti wa sasa Ndugu Juma Mohamed Kibanda juu ya tatizo la mradi huo kufika huko alisema”hii inatokana na usimamizi mbovu wa uongozi uliopita madarakani ,uongozi kukosa uwazi na uwajibikaji jambo ambalo limepelekea mradi huu wa maji safi na salama kufa na wananchi wetu kuangaika”
Baadhi ya mfumo wa mabomba ya maji yamepasuka kusabisha maji mengi kuvuja na kusambaa maeneo mbalimbali ya mtaa, na kusababisha uchafuzi wa mazingira katika maeneo hayo ambapo ni hatari kwa afya ya jamii iliyo zunguka maeneo hayo.
Uongozi utambue wananchi wako katika mazingira hatarishi ya kiafya na hata upatikanaji wa maji safi na salama hivyo iwe ni changamoto kwao ili kutafuta ufumbuzi wa tija kuondoa tabu hiyo.



Na; Joseph malisa 

No comments: