Translate
Translate
Saturday, 18 April 2015
BARABARA ZA JAZWA VIFUSI VYA MATOPE MTAA WA MAKANGARAWE WILAYA YA TEMEKE
Juhudi za maendeleo mtaa wa Makangarawe Wilaya ya Temeke Jijini Dar es salaam Serikali imejaza vifusi barabara za mtaa wa Makangarawe jinsi ambavyo wananchi wa maeneo hayo wakilalamika kuwa vifusi hivyo ni matope matupu kipindi cha mvua zikianza kunyesha.
Juhudi hizo za serikali ziliongozwa na mwenyekiti wa mtaa kuhakikisha zoezi ilo linakamilika.
Hitambulike kuwa fedha zinazotumika katika ujenzi huu ni fedha za wananchi hivyo kuweka vifusi ambavyo vinaongeza gharama ni ufujaji wa fedha za umma pasipo malengo, Ni wazi kabisa uwekaji huu wa vifusi ni wakibabaishaji ambao matokeo yake ni matumizi mabaya ya fedha.
Wananchi wanahaki wa kukemea jambo kama ili na kuligomea ili kuonesha msimamo wao ili mambo kama haya ya matumizi mabaya ya fedha yasijitokeze kama serikali inaamuwa kuweka vifusi barabara za mtaa basi hihakikishe inaweka kifusi cha uhakika na cha kudumu chenye mwendelezo kuliko kuweka matope ambayo na chafuzi katika mazingira yetu
Wananchi inawapasa watambue MATUMIZI MABAYA NI UBADHILIFU hivyo vipigwe vita tabia hii.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment