Translate

Translate

Wednesday, 7 January 2015

MAMBO KUMI NA MOJA YA KUZINGATIA KABLA YA KUFANYA PETS (VIEW BLOG)

UTARATIBU WA WANANCHI KUENDESHA PETS
MASUALA YA KUZINGATIA KABLA YA KUFANYA PETS
·      Unda kamati au kikundi cha PETS inayojumuisha uwakilishi wa makundi yote wakiwemo wanawake na vijana.
·      Ainisha/bainisha sekta husika kwa ajili ya ufatiliaji
·      Bainisha namna ya kufuatilia na kupata taarifa za kutosha kuhusu hali halisi ya sehemu husika kabla ua ufatiliaji
·      Zingatia jinsi/namna ya kufanya ufuatiliaji
·      Tambua wapi pa kwenda kwa ajili ya kupata taarifa husika
·      Nini / kitu gani cha kuuliza
·      Nini kifanyike kuhamasisha umma
·      Jinsi ya kutoa mrejesho na kusambaza taarifa
·      Hatua za kuchukua (ushawishi na utetezi)
·      Kitu gani au nini kimebadilika?

·      Vyanzo mbalimbali vya taarifa (TAKUKURU, TAMISEMI nk)

Tuesday, 6 January 2015

MALENGO YA UFUATILIAJI- PETS

PETS imethibitika kuwa ni kati ya zana na nyenzo muhimu katika ufuatiliaji wa matumizi ya rasilimali za umma , hasa pale inapofanyika kwa mitizamo wa kijinsia . Hivyo basi , PETS inalenga kufanikisha yafuatayo;

Ø Kuboresha utoaji huduma ; kufuatilia matumizi ya fedha au rasilimali za umma kwa mtizamo wa kijinsia , kunasaidia sana kuchochea uboreshaji wa utoaji wa huduma mbalimbali za kijamii kwa ubora uliokusudiwa . vile vile kuhakikisha kuwa rasilimali zimeenda kutekeleza lengo kusudiwa na kuhakiki thamani halisi ya fedha zilizotumika.
Ø Kuhakiki utendaji wa serikali na mamlaka husika; mfumo huu unasaidia sana katika kuhakiki utendaji wa serikali na mamlaka husika ,hasa katika ngazi za vitongoji na vijiji au katika vikundi vidogo vidogo , kwa kusoma nyaraka , ripoti na taarifa mbalimbali za utekelezaji.
Ø Kukuza uwajibikaji;  Hii inaanzia kwa wananchi kwa maana ya wanawake , wanaume , vijana , walemavu na makundi mengine yaliyoko pembezoni , ambapo hushiriki moja kwa moja katika kuhoji serikali .sanjali na hilo huhakikisha kwamba viongozi wanatenda kila ambacho wanapaswa kutenda kulingana na mipango.
Ø Kuwezesha uandaaji wa mipango shirikishi ya maendeleo;  Taarifa zinawafanya wananchi waweze kushiriki vizuri katika uandaaji wa mipango ,au katika kubaini aina ya miradi itakayotekelezwa kwenye jamii hisika


Friday, 2 January 2015

JE? TANZANIA INA UTAWALA BORA click usome kujua nini utawala bora

UTAWALA BORA
Utawala bora ni matumizi ya uwezo (mamlaka)wa kiserikali katika jitihada za kuongeza na kutumia rasilimali hizo ili kuboresha maisha ya wananchi
MISINGI YA UTAWALA BORA
v      Utawala wa kidemokrasia
v      Ushirikishwaji wa umma
v      Utawala wa kisheria
v      Haki na usawa kwa watu wote
v      Uwazi katika kuendesha shughuli za maendeleo
v      Uwajibikaji katika utendaji
v      Uadilifu
Misingi hii ikizingatiwa na kufanyiwa utekelezaji lazima mabadiliko yataonekana

Ili utawala bora uwe na sifa za kupendeza na kuendwa na wananchi lazima uzingatie Misingi ya utawala bora.

TEC MEDIA vs YOUTHCAN VIDEO

SOMA UFAHAMU KWA KINA JUU YA KAMATI ZA SERIKALI ZINAVYOKWENDA KINYUME NA SHERIA ZA NCHI kwa faida yetu sote

KAMATI  ZA HALMASHAURI YA KIJIJI/KAMATI YA MTAA

Ø Kuna kamati tatu za halmashauri ya kijiji/mtaa kisheria
Ø Kamati ya fedha,mipango na uchumi ,huduma za jamii na shughuli za kujitegemea na ulinzi na usalama
Ø Mkutano mkuu wa kijiji/mkutano wa wakazi wa mtaa una uwezo wa kuagiza halmashauri ya kijij/kamati ya mtaa kuundaa kamati ya muda kwa shughuli maalum au halmashauri yenyewe inaweza kuunda kukiwa na haja ya kufanya hivyo.
Ø Idadi ya wajumbe katika kamati inashauriwa wasipungue wajumbe watatu 3 na wasizidi wajumbe watano 5
Ø Kamati za kisheria inafaa ziongozwe na mjumbe wa halmashauri ya kijiji /kamati y mtaa
Ø Inashauriwa wenyekiti wa kijiji /mtaa , wenyeviti wa vitongoji  wasiwe wenyeviti wa kamati mbalimbali ili kutolimbikiza madaraka yote kwa halmashauri ya kijiji/kamati ya mtaa
Ø Wananchi  wakaida wanaweza kuwa wajumbe wa kamati au wanaweza kuitwa kutoa ushauri kwenye vikao vya kamati
Ø  Kamati zinaweza kukutana mara kwa mara kutunza kumbukumbu na kuendesha vikao kwa kushauriwa na afisa mtendaji wa kijiji (VEO)/ Afisa mtendaji wa mtaa(MEO)

Thursday, 1 January 2015

JE? WAJUA WAJIBU WETU KWENYE SERIKALI ZA MTAA/KIJIJI? soma kwa utulivu utagundua mapungufu yetu na ya serikali usika

Mwananchi ana wajibu na majukumu yake kuhakikisha kuwa kiongozi aliyemchagua au kuteuliwa anatimiza wajibu wake ipasavyo katika viwango vinavyokubalika katika eneo la kijiji/mtaa kulingana na mipango na makibaliano ya vikao vya kisheria ya kijij na mtaa.
Kila mwananchi ana wajibu wa kupinga na kukataa kila aina ya uovu kayika jamii ikiwemo rushwa,uonevu wizi ubadhilifu wa mali za umma nay a watu binafsi.

Wananchi pia wana jukumu la kudai na kupigania haki zao na za wananchi wengine kutoa malalamiko na kuuliza maswali juu ya mambo mbalimbali yananoendelea kijijini au kwenye mtaa kupitia vyombo mbalimbali vya kijamii na kiserikali. Wananchi wanashiriki katika serikali za mitaaa kupitia vikao au mikutano mbalimbali ambapo hujadili na kutoa mapendekezo  yao kuhusu mipango na matatizo yanayowakabili kwa mamna moja au nyingine ili kuweza kupatiwa ufumbuzi na kurahisisha uboreshaji wa huduma za kijamii katika maeneo yao wanamoishi.