Translate

Translate

Saturday, 26 April 2014

MKUKUTA NI NINI?soma ujilidhishe

MKUKUTA ni nini?NI kifupisho cha maneno ya Kiswahili yenye maana ya mkakati wa kukuza uchumi na kupunguza umasikini Tanzania.
MKUKUTA awamu ya 1(2005/06-2009/10)ulilenga katika kukuza uchumi ,kupunguza umasikini wa kipato ,ubora wa maisha ya watu na ustawi wa jamii pamoja na kuimarisha utawala bora na uwajibikaji .utekelezaji wake ulienda sambamba na uandaaji wa ripoti za kila mwaka zikiainisha uzoefu ,mafanikio na changamoto.
Kila mwaka ripoti zilijadiliwa na wadau mbalimbali katika makongamano na mikutano ya kitaifa ya sera.Maoni kutoka kwenye mapitio na mijadala hiyo yalitumika katika kuboresha mpango wa mwaka uliofuata.
MKUKUTA inachangia katika utekelezaji wa dira ya taifa ya maendeleo(2025)na malengo ya maendeleo ya millennia (2015).

Tuesday, 15 April 2014

SOMA UJUE VYANZO VYA HAKI VYA MWANANCHI WA TANZANIA

HAKI ZA UHALALI WA MWANANCHI KUFATILIA MATUMIZI YA RASILIMALI ZA UMMA(PETS)
Haki ni stahili ya binadam .Hii inamaanisha kuwa mtu ana haki kwa kuwa anastahili ya kutenda jambo Fulani,au wengine wanatakiwa kutenda au kumtendea jambo Fulani katika hali Fulani . Haki zinaweza kuwa binafsi au za jumla . Kwa lugha rahisi ,tunasema kuwa haki ni stahili za msingi ambazo binadamu yeyote Yule bila kujali jinsia ,umri ,itikadi,dini,rangi ,kabila au aina yoyote ya utofauti huzaliwa nazo na hazitolewi na mtu na wala haziwezi kuondolewa na mtu kwa sababu yeyote .vivyo hivyo ,uhalali wa mtu kufanyanya au kufanyiwa jambo Fulani ,unatikana na stahili ambayo mtu au wattu wanakuwa nayo kw mujibu wa sheria ,sera kanuni ,taratibu au muongozo husika,Ni kwa muktadha huo,wananchi kupitia sheria ,sera,matamko ,mikataba ,kanunui na miongozo mbalimbali ,wanapata haki na uhalali wa kufuatilia matumizi ya rasilimali za umma kila mara wanapoona inafaa kufanya hivyo

                 NB;VYANZO VYA HAKI
a)mila na desturi
b)katiba ya nchi
c)sera na miongozo
c)sheria za nchi
d)kanuni na mikataba ya kitaifa /kimataifa

Saturday, 12 April 2014

MIFUMO YA TATHIMINI NA UFATILIAJI WA RASILIMALI ZA UMMA(PETS)

Kuna aina kadhaa za mifumo ya tathmini ambayo inatumiwa kulingana na mahitaji au mazingira ya sehemu husika.mifumo hiyo ni kama vile;ufatiliaji wa Matumizi ya fedha za umma(public expenditure system and survey),ushirikishwaji wa jamii ya vijiji katika tathmini(participatory rural appraisal(PRA),tathmini ya uwajibikaji wa jamii(social accountability monitoring)na PIMA KADI
Mifumo yote hiyo imeainishwa utaratibu ambao unaweza kutumika katika kukusanya taarifa inayokusudiwa katika kuijenga jamii uwezo,kuiwezesha kuwa na kauli na kushiriki ipasavyo katika kutathimini na kuiwajibisha mamlaka husika pale inapobainika kuwa rasilimali za umma zimetumika  kinyume na jinsi ilivyokusudiwa.Mifumo yote hiyo ni sahihi na inafaa kutumika kilingana na chaguo la sehemu husika.
Katika muongozo huu ,mfumo mkuu wa tathmini utakaotumika na tutakaojikita nao zaidi ni mfumo wa ufatiliaji wa matumizi ya fedha za umma au PETS,pia tutaangalia kwa undani kuhusu zana ya PIMA KADI na jinsi inavyotumika kama nyenzo ya kukusanya taarifa.
Kwa ujumla PETS na mifumo yake imesaidia kujibu maswali ambayo mara nyingi wananchi wamekuwa wanajiuliza ili kupima tathimini ya fedha zilizopangwa au kutumika na matokeo husika .Hivyo kupitia PETS wananchi wanaweza kufanya tathimini na kupata ufumbuzi wa maswali yanayowakabili kuhusu mgawanyo wa matumizi ya rasilimali zao. Baadhi ya maswali ambayo wananchi hujiuliza ni kama yafuatayo
1)je,fedha na rasilimali za umma huwafikia wananchi hususani wale wa ngazi ya chini mfano wanawake na watoto kama ilivyokusudiwa ?
2)je,rasilimali fedha na rasilimali zingine zinawafikia wananchi kwenye maeneo husika kwa mtizamo wa kijinsia?
Utaona kuwa swali la kwanza linalohoji mtiririko wa fedha na rasilimali za umma zitolewazo ama na serikali kuu au wafadhili au wabia wa kimaendeleo ili kugharamia miradi ya maendeleo katika kijiji,kata.Mantiki yake ni kutaka kufahamu ni kiasi gani cha fedha na rasilimali za umma zimewafikia walengwa au watoa huduma,kama vile hospitali,shule ,maji ,barabara  nk kama ilivyokusudiwa.
Katika kufanya tathmini na kujiuliza maswali hayo ,na iwapo kuhoji huko kunaweza kukasababisha uchunguzi na ikadhihirika kuwepo na utofauti ya fedha zilizotolewa katika ngazi ya serikali kuu na kiasi kilichopelekwa kwa watoa huduma katika ngazi za nchini,huo unaitwa uvujaji.Hii inamaanisha kuwa baadhi ya pesa au rasilimali zilizotolewa kwa ajili ya miradi ya maendeleo,hazijatumika kulingana na sera au maleng yaliyokusudiwa na serikali au mamlaka husika.maana yake ni kuwa fedha au rasilimali hizi zimekwapuliwa katika ngazi Fulani ya kiutawala,inaweza kuwa wilayani au mikoani.
Hali kadhalika ,swali la pili linalenga zaidi katika uchambuzi.Lengo ni kubainisha kwa nini uvujaji hujitokeza.Mara nyingi,hujibu maswali kama vile ,kwa nini uvujaji hutokea katika baadhi ya halmashauri zaidi ya zingine?Au kwa nini shule ,halmashauri kadhaa hupokea fedha na rasilimali nyingi kuliko zingine
Kwa kufanya utambuzi huo ,mfumo unawezesha namna ya kufatilia ili kupunguza uvujaji na kuboresha utendaji na uwajibikaji katika ngazi ya ki-serikali /uongozi /utawala husika
Hivyo basi,ili kuondosha mianya ya rushwa na kuimarisha utawala bora katika ngazi zote husika za uongozi,ni vyema kutambua mianya ya rushwa,ambapo suala la kuwajengea uwezo wananchi au wapokeaji wa huduma,litaweza kusaidia usimamizi na udhibiti wa rasilimali katika maeneo yote.Pia kwa kutumia mfumo wa PETs wananchi watadai taarifa za matumizi kulingana na huduma zitolewazo ,pia watahoji kiwango cha utendaji kazi wanapokuwa na shaka ,hivyo kuzuia kushamiri kwa rushwa kwa viongozi wao.

Wednesday, 9 April 2014

UTAWALA WA KIDEMOKRASIA KATIKA JAMII NINI?soma ufahamu.

Mwananchi ana wajibu na majukumu yake kuhakikisha kuwa kiongozi aliyemchagua au kuteuliwa anatimiza wajibu wake ipasavyo katika viwango vinavyokubalika katika eneo la kijiji/mtaa.Kila mwananchi ana wajibu wa kupanga na kukataa kila aina ya uovu katika jamii ikiwemo rushwa,uonevu,wizi,ubadhilifu wa mali za umma nay a watu binafsi.
Mwananchi pia wana jukumu la kudai na kupigania haki zao za wananchi wengine kutoa malalamiko na kuuliza maswalijuu ya mambo mbalimbali vya jamii na kiserikali.Wananchi wanashiriki katika serikali za mitaa kupitia vikao au mikutano mbalimbali ambapo hujadili na kutoa mapendekezo yao kuhusu mipango na matatizo yanayowakabili kwa namna moja au nyingine ili kuweza kupatiwa ufumbuzi na kurahisiha uboreshaji wa huduma za kijamii katika maeneo yao wanamoishi.



TUNGEIJUA 
VIZURI SOMO LA DEMOKRASIA TUNGEIPIGANIA MPAKA VIONGOZI WAIFATE IPASVYO

Monday, 7 April 2014

SAFISHA JIJI TANDIKA SOKONI WAKIMBIZANA NA MIZIGO tazama picha


Operesheni ya safisha jiji katika mji wa dar es salaam umekuwa gumzo kubwa sana katika maeneo mbalimbali jijini dar es salaam baada ya wafanyabiashara kukimbizana na mizigo yao ili kuepusha shari ya serikali,
katika eneo la Tandika sokoni jana asubuhi wafanyabiashara hao ambao waliweka biashara zao katika maeneo yasiyo sahihi walikumbwa na operesheni hiyo ya kusafisha jiji,pia katika maeneo ya mbagala safisha jiji ilifanyika kupitia jeshi la polisi likisaidiaana na jeshi la wagambo.


Friday, 4 April 2014

JE? NI KWELI JAMHURI YA MUUNGANO INAENZI NA KUZINGATIA TUNU HIZI soma uzijue tunu za Taifa

JAMHURI YA MUUNGANO ITAENZI NA KUZINGATIA TUNU ZA TAIFA ZIFUATAVYO:
a)utu;
b)azalendo;
c)uadilifu;
d)umoja;
e)uwazi;
f)uwajibikaji ;na

g)lugha ya Taifa.

SOMA KWA MAKINI UTANGULIZI HUU WA RASIMU YA JAMHURI TA MUUNGANO WA TAZANIA

Kwa kuwa, sisi wananchi wa jamhuri wa muungano wa Tanzania tumeamua rasmi na kwa dhati kujenga katika nchi yetu jamii inayoheshimu na kuzingatia misingi ya utu,uhuru,haki,usawa,udugu,amani,umoja na mshikamano katika Nyanja zote za maisha yetu;


Na kwa kuwa,tunaamini kuwa misingi hiyo inaweza tu kutekelezwa katika jamii yenye mfumo wa kidemokrasia na utawala bora ambayo serikali yake inasimamiwa na Bunge lenye Wabunge waliochaguliwa na wanaowakilisha wananchi,na Mahakama huru zinazotekeleza wajibu wa kutoa haki bila woga wala upendeleo kudumisha na kwamba wajibu wa kila mtu unatekelezwa kwa uaminifu
Na kwakuwa ,tunatambua umuhimu wa kutunza mali ya mamlaka ya nchi na pamoja,kupiga vita aina zote za uharibifu,ubadhirifu na kuhimiza matumizi bora na endelevu ya rasilimali na mustakabali wa maisha ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo;
Na kwa kuwa,tunatambua umuhimu na faida za kujenga,kukuza na kuendeleza amani,umoja,urafiki na ushirikianao  miungoni mwa watanzania,mataifa mbalimbali ya Afrika na duniani kwa ujumla;
Na kwa kuwa,azma ya kujenga umoja wa bara la Afrika inadhihirishwa na Muungano wa iliyokuwa jamhuri ya Tanganyika na jamhuri ya watu Zanzibar;
Na  kwa kuendeleza dhamira yetu hiyo,ni muhimu:
a)kulinda,kuimarisha na kuudumisha muungano wa  nch za jamhuri ya Tanganyika na jamhuri ya watu wa Zanzibar;
b)kujenga Taifa huru na linalojitegemea;
c)kuimarisha na kuendeleza utawala wa sheria;
d)kukuza na kuendeleza maadili,uwajibikaji na uwazi;
e)kujenga umoja na mshikamano utakaowezesha kutimiza malengo ya kisiasa,kiuchumi ,kijamii,kimazingira na kulinda urithi kwa ujumla;
f)kujenga na kuendeleza ukuu wa mamlaka ya watu;
g)kujenga na kuendeleza utii wa mamlaka ya katiba;na
h)kuimarisha na kudumisha uzalendo kwa taifa miungoni mwa watanzania;
NA KWA KUZINGATIA,urithi tulioachiwa wa waasisi wa Taifa letu wa kujenga nchi yenye umoja wa watu wake ambao hawabaguani kwa misingi ya ukabila,dini ,rangi,jinsi au ubaguzi wa aina nyingine yoyote;
NA KUZINGATIA,uzoefu wa zaidi ya miaka hamsini ya uhuru wa Tanganyika,miaka hamsini ya mapinduzi ya Zanzibar na miaka hamsini ya muungano wa jamhuri ya Tanganyika na jamhuri ya watu wa Zanzibar,na uhumuhimu wa ushiriki mpana na bayana wa wananchi katika utungaji wa katiba ya jamhuri  ya muungano wa Tanzania;
HIVYO BASI,KATIBA HII YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA ILIYOPENDEKEZWA NA BUNGE MAALUM LA KATIBA imetungwa na SISI WANACHI WA JAMHURI YA MUUNGANO WATANZANIA kupitia KURA YA MAONI kwa madhumuni ya kujenga jamii kama hiyo,na kuhakikisha kuwa jamhuri ya muungano wa Tanzania inaongozwa na serikali yenye kufuata misingi ya demokrasia na utawala wa sheria,kujitegemea na isiyofungamana na dini.



 TOA MAONI YAKO

Wednesday, 2 April 2014

JE?UNAWAZO GANI KATIKA HILI?UNAWAAMBIA NINI KATIKA KUTUNZA MAZINGIRA?tazama picha katika jiji la Arusha jinsi mitalo ya maji inavyokuwa kero kwa afya

Ni wazi kabisa tunatambua hili ni tatizo kubwa ingawa linachukuliwa kawaida sana,katika haki za binadamu lazima tuzingatie na mazingira yake anayoishi.



Mradi wa barabara umeletwa katika jamii ni jambo zuri sana lakini inakuwa mbaya sana kama barabara hizo zinatengenezwa bila kukamilika kabisa hii ni kuchezea fedha za umma

Hizi picha ni katika jiji la Arusha asilimia kubwa sehemu nyingi mitalo haijafunikwa kabisa jambo ambalo linasababisha kuchafua mazingira ya jiji.

weka mazingira safi ili yakuweke safi