Translate

Translate

Friday, 29 November 2013

MALENGO YA UFUATILIAJI-PETS

PETS imethibitika ni kati ya dhana na nyenzo muhimu katika ufuatiliaji wa matumizi ya rasilimali za umma,hasa pale inapofanyika kwa mtizamo wa kijinsia.Hivyo basi,PETS inalenga kufanikisha yafuatayo;
1)kuboresha utoaji huduma
2)kuhakikisha utendaji wa serikali na mamlaka husika
3)kukuza uwajibikaji
4)Kuwezesha uandaaji wa mipango shirikishi ya maendeleo

Wednesday, 27 November 2013

MCHANGO WA DINI MBALIMBALI KATIKA KUTEKEKELAZAJI PETS

PETS kama dhana moja wapo wa ufatiliaji wa matumizi ya rasilimali za umma,inasukumwa na lengo kuu la kuona kuwa rasilimali za umma zinztumika ipasavyo na kwa mgao unaowiana ili kuleta maendeleo kwa makundi yote ya jamii.Mafnikio ya PETS kwa kiasi kikubwa yanategemea ushirikiano wa karibu baina ya vyombo , taasisi ,asasi,vikundi na makundi mbalimbali katika jamii ambapo yote kwa pamoja wanahusika katika kusimamia rasilimali za umma ili kuona maendeleo na ustawi wa jamii.

VIONGOZI WA DINI wananafasi kubwa sana katika masuala ya kiroho,pia dini zina wajibu mkubwa sana wa kuchangia katika masuala ya kawaida ya kibinadamu,hasa katika shughuli za ki- maendeleo na uchumi ili kuwasaidia waumini kukabiliana ba changamoto za maisha.DINI kama sehemu ya jamii ,zina wajibu na majukumu makubwa ya kushauri,kuelekeza,kuonya,kufundisha na kukemea mienendo yoyote isiyofaa na hasa inayokinzana na misingi yaUADILIFU,UWAJIBIKAJI,USAWA,na HAKI hivyo kuhamasisha waumini kumcha MUNGU ili kukomesha uharibifu na ubadhilifu na kusimamia vyema rasilimali za umma ili ziwe na faida kwa wote.
 MAENDELEO HAYANA DINI WALA KABIRA WOTE TUNAHATHIRIKA NA UBADHILIFU UNAO JITOKEZA HIVYO KWENYE MASUALA YA MAENDELEO WOTE WAMOJA.
   
ASANTE

JOSE MALI: JINSI JAMII INAVYOPOKEA VIZURI ELIMU YA PETS MKOAN...

JOSE MALI: JINSI JAMII INAVYOPOKEA VIZURI ELIMU YA PETS MKOAN...: wananchi wa karoleni moshi kilimanjaro wakitafakari  baada ya mafunzo ya PETS Baada ya vijana kutoka TAASISI mbalimbali ...

JINSI JAMII INAVYOPOKEA VIZURI ELIMU YA PETS MKOANI KILIMANJARO



wananchi wa karoleni moshi kilimanjaro
wakitafakari 
baada ya mafunzo ya PETS




Baada ya vijana kutoka TAASISI mbalimbali za dini kuweza kutoa elimu ya ufatiliaji wa matumizi wa rasilimali za umma, wananchi wamebaki wakitafakari kwa kina jinsi ya kufanya na wapi waanzie ili kujiridhisha na serikali yao.

Saturday, 23 November 2013

PATA NAKALA YAKO BURE CHA KITABU CHA MUONGOZO WA UFATILIAJI NA USIMAMIZI WA MATUMIZI YA RASILIMALI ZA UMMA KWA MWANANCHI

PETS public expenditure tracking system/survey
hiki ni kitabu kizuri ukikisoma kitakufindisha mambo mengi sana,ni raisi kukipata kwa ajili ya kujifunza ufatiliaji hivyo unaweza kukipata kwa urahisi pia wasiliana nami kupitia namba hii 0712064800

Friday, 22 November 2013

JE?UNAJUA RANGI AU KAVA LA KATIBA JINSI LILIVYO

Tusije tuka piga kelele eti katiba ibadilishwe nakati ujui hata katiba ilivyo si kwamba nawaponda hapana bali katika harakati hizi za kubadilisha mfumo mzima wa nchi kwa ajili ya maendeleo basi tujitahidi kujuwa haki zetu na wajibu wetu katika maendeleo tunayoyataka.
                                                                                                                                                                    KATIBA YA YETU
inapatika kwenye maduka ya serikali.                  

Sunday, 17 November 2013

HOTUBA YA MHESHIMIWA KASSIMU MAJALIWA(MB)NAIBU WAZIRI WA TAMISEMI KATIKA UFUNGUZI WA MDAHALO WA KITAIFA WA DINI MBALIMBALI JUU YA USIMAMIZI WA RASILIMALI ZA UMMA TAREHE 30/05/2013 KATIKA UKUMBI WA BLUE PEAR-DAR ES SALAAM.

Ndugu mkurugezi wa baraza la dini mbalimbali za dini Tanzania;
Ndugu washirika wa maendeleo,
Ndugu maafisa wa serikali,        
Ndugu wawakilishi wa mashirika ya kiraia,
Ndugu wawakilishi kutoka kamati za PETS vijijini,
Ndugu wanahabari,
Wageni waalikwa,
Mabibi na mabwana.


Ndugu mkulugenzi;
Awali ya yote napenda nitumie nafasi hii kwanza kumshukuru mwenyezi Mungu ,kwa kutupa uzima,afya,nguvu ,na kibali cha kutuwezesha kukutana katika tukio hili muhimu .Nilishukuru pia baraza la dini mbalimbali nchini kwa kuhakikisha tukio hili muhimu linafanyika ili tuweze kuzungumzia masuala mbalimbali muhimu kuhusu mstabali wa maendeleo ya wananchi .Nashukuru pia kwa maamuzi yenu ya kuialika TAMISEMI katika shughuli hii kwani kwa kweli sisi ndio wenye dhamana kubwa na shughuli mbalimbali zinzzomlenga mwananchi wa kawaida .Ndio maana pamoja na majukumu tuliyo nayo BUNGENI kwa sasa lakini baada ya kupata mwaliko wenu tumefanya maamuzi ya kuweza kushiriki.Niwape pole pia washiriki mbalimbali waliotoka nje ya Dar es salaam kwa safari ndefu kutoka sehemu mbalimbali kuja hapa kushiriki kongamano hili muhimi.

Ndugu washiriki,
Napenda pia kutambua mchango na kutoa shukrani za dhati kwa wadau mbalimbali wamaendeleo na Taasisi mbalimbali kwa kuwezesha maandalizi ya shughuli hii kufanyika wakiwemo Baraza kuu la waislam Tanzania (BAKWATA,)jumuiya ya wakristo Tanzania(CCT),Baraza kuu la maaskofu katoliki  Tanzania (TEC),Kanisa la kiinjili la kilutheli Tanzania ,shirika la kikristu linalotoa huduma kwa wakimbizi Tanganyika(TCRS),Shirika la shughuli za maendeleo ya wanawake (WIA)pamoja na shirika la maendeleo la Norway(NCA).Mchango wenu ni mkubwa sana katika kusukuma gurudumu la MAENDELEO kwa wananchi na kwa Taifs kiujumla ,ninatambua kuwa na ushirka wa madhehebu ya dini katika kuchangia maendeleo nchini ni wa kihistoria.Ninapenda kuwapongeza zaidi kwa kuwa sasa sit u mnatukumbusha kuwajibika kupitia ibada mbalimbali bali pia mnashiriki katika kuelimisha jamii hata nje ya nyumba za ibada.Lakini kwa namna ya pekee zaidi napenda kuwapongeza kwa kuwa tunapata fursa ya kutafakari  juu ya wajibu wetu katika kuleta maendeleo endelevu.

Ndugu Mkurugenzi na Washiriki,
Mandeleo ya nchi yanawezekana endapo kila mmoja wetu mahali alipo atatizama wajibu wake kwa malengo na bila kusukumwa. Malengo ndio msingi mkubwa katika utendaji kazi.Kwa watumishi wa umma,pamoja na malengo mengine lengo kuu ni kuhakikisha kuwa wanawatumikia wananchi kwa kadri ya uwezo ,kujituma na kuwa waaminifu na wabunifu katika kutumia rasilimali zilizopo kwa ufanisi.Sote tunafahamu kuwa hakuna siku ambayo mtu atasema rasilimali zilizopo zinamtosheleza.lakini ni imani yangu kwamba,rasilimali ndogo zilizopo zikitumika vema zinaweza kuleta mabadiliko katika undendaji na baadae kuleta maaendeleo makubwa ya Taifa na wananchi kwa ujumla .Tangu kupata uhuru,serikali imekuwa ikifanya jitihada kuhusu kuhakikisha kuwa huduma bora zinawafikia wananchi.katika kufanikisha jambo hili,serikali imekuwa ikichukuwa hatua mbalimbali ikiwemo kuanzishwa kwa mpango wa uboreshaji wa serikali za mitaa ulioanza mwaka1998 ambao unalenga katika kupeleka madaraka kwa wananchi.Lengo la kuwa na maboresho ni kuhakikisha kuwa mamlaka za serikali za mitaa zinapewa uhuru wa kufanya maamuzi mbalimbali yahusuyo utoaji wa huduma kwa wananchi na kuwakilisha wananchi katika kujiletea Maendeleo na ustawi wao kwa ujumla.

Ndugu Mkurugenzi na Washiriki,
Kwa mujibu wa sharia ya serikali za mitaa sura ya 287,majukumu ya mamlaka za serikalia za mitaa ni pamoja na kudumisha amani,usalama ,utulivu na kutoa huduma bora za jamii na kiuchumi kwa wananchi ,kutekeleza shughuli za maendeleo pamoja na kupanga mipango ya maendeleo  endelevu.Aidha ,serikali inazingatia sana suala la ushirikishwaji wa wananchi katika mipango mbalimbali na utekelezaji wa wananchi katika mipango mbalimbali na utekelezaji wa shughuli za maendeleo.Hili linafanyika kwa kuzingatia Mpango wa fursa na vikwazo kwa Maendeleo (opportunities and obstacles to Development-O&OD).Mpango huu ulianzishwa na serikali sambamba na awamu ya pili ya program ya maboresho ya serikali za Mitaa(2002)kwa lengo la kusaidia jamii kuwa na uelewa mkubwa kuhusiana na umiliki wa mchakato wa maendeleo.Maelekezo ya kuwashirikisha wananchi katika shughuli za maendeleo ni ya lazima na maendeleo,sharia za fedha na hata katiba ya nchi.

Ndugu Mkurugenzi na washiriki,

Dhana na lengo  la kuwa na ufuatiliaji wa Matumizi ya Rasilimali za Umma kwa wananchi ni suala muhimu katika kuhakikisha rasilimali za Nchi zinatumika ipasavyo na hatimaye kuboresha huduma za jamii. Sote tunafahamu panapotokea kufujwa,kuharibiwa au kupotea kwa rasilimali za umma ambazo zilipangwa katika kuendeleza utoaji wa huduma kwa wananchi ,watu wote huathirika bila kujali dini,kabila rangi au eneo.Hivyo basi ili kuwa na uhakika wa matumizi mazuri ya rasilimali hizo,wananchi wote bila kujali tofauti zao za kiimani,hawana budi kuungana na kushirikiana pamoja katika ufuatiliaji wa mapato ya matumizi ya rasilimali zao.  Serikali inatambua na kuthamini  jitahada zinazofanywa na umoja wenu katika kutekeleza miradi ya kuijenga uwezo jamii kushiriki kufuatilia mapato na matumizi ya rasilimali za Umma katika wilaya takribani 25 Tanzania bara na visiwani.Nakiri kuwa yapo mafanikio kutokana na baadhi ya viongozi  wasiowajibika katika kuwa mafunzo  yenu yamewezesha kwa kiasi kikubwa kujenga uwajibikaji na kuboresha utolewaji wa taarifa na huduma katika maeneo mbalimbali.Azma ya serikali ni kuendelea kutoa ushirikiano nanyi wakati wote.

Ndugu Mkurugenzi na Washiriki,
Napenda nitumie fursa hii kutoa wito kwenu na jamii kwa jumla kuendelea kutoa ushirikiano kwa kuwabaini baadhi ya viongozi wa Halmashauri na vijiji wasio waaminifu wanaochangia kurudisha nyumba juhudi za kuleta maendeleo kwa kujinufaisha binafsi.Wapo  viongozi waliopewa dhamana ya kusimamia rasilimali za umma ikiwepo fedha za uendeshaji wa shule,huduma ya afya na pembejeo za kilimo lakini hawazifikishi katika maeneo husika.Ninapenda kuwatia moyo wanakamati za PETS pamoja na jamii kwa jumla kutokana tama pale wanapoona viongozi wachache wasio waadilifu wanatumia vibaya madaraka yao kujinufaisha binafsi. Jambo la msingi ni kuzingatia kuwa Nchi yetu inaongozwa kwa msingi ya sheria na Utawala bora. Hivyo tuepuke kujichukulia sheria mkononi au kufanya maamuzi yanayopaswa kuamuliwa  kisheria.Tumieni vyombo vinavyohusika na wahamasisheni  wananchi kuzingatia sheria  za Nchi  pale yanapojitokeza mapungufu kwa watendaji wa serikali na kwa jamii kwa ujumla.Vipo vyombo kama vile Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa –TAKUKURU na Jeshi la polisi,vitumieni  ili watuhumiwa washughulikiwe kwa mujibu wa sheria.Viongozi wa vijiji na Halmashauri zote nchini  wanao wajibu wa kutoa ushirikiano wa dhati na wakati wote milango yetu ipo wazi kwa ajili ya kupokea ushauri na maoni yenu.

Ndugu washiriki,
Mwisho napenda kuwasisitiza juu ya umuhimu wa kuendelea na kuhamasisha umoja wa Taifa letu hasa katika kipindi hiki ambacho baadhi ya watu wameanza kupandikiza hisia za udini kwa wananchi kwa malengo binafsi.Nchi hii ni yetu sote na wote tunawajibika kuuenzi mshikamano ambao tumekuwa nao  katika kipindi chote tangu tulipopata uhuru.  Umoja na Amani tulivyonavyo ni msingi ambayo waasisi wa Taifa hili wametuachia kama urithi wa pekee kabisa.Navikikosekana vitu hivi dhana nzima ya maendeleo kwa wananchi wetu itakuwa ni ndoto.  Ninafahamu wote tunatambua changamoto zilizotokea katika nchi za jirani na jinsi ambavyo watoto na kina mama wasio na hatia walivyoathirika na wengine kupoteza maisha.Naomba wote kwa pamoja tuwe walinzi wa Amani na Utulivu tulio nao. Vitu hivi vikitoweka sisi sote bila kujali DINI,KABILA NA RANGI zetu tutapata madhara makubwa sana.
Nimalize kwa kuwatakia Mdahalo wenye mafanikio katika kukuza uwezo wa wananchi kufuatilia Matumizi ya Rasilimali za Umma kwa kuleta maendeleo kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.
Baada ya kusema haya machache napenda nitamke kuwa kongamano hili limefunguliwa rasmi.

                                           ASANTE SANA

Friday, 8 November 2013

josemali: SIFA ZA KAMATI YA PETS

josemali: SIFA ZA KAMATI YA PETS: 1)umri wa wanakamati;wawe wa umri tofauti kamati inaweza kuwa na mchanganyiko wa vijana na wazee 2)jinsia;kamati izingatie uwakilishi sawa ...

SIFA ZA KAMATI YA PETS

1)umri wa wanakamati;wawe wa umri tofauti kamati inaweza kuwa na mchanganyiko wa vijana na wazee
2)jinsia;kamati izingatie uwakilishi sawa wa watu wa jinsia zote wanawake na wanaume
3)dini mbalimbali;kamati iwe na uwakilishi wa watu kutoka dini mbalimbali zilizopo katika eneo
4)uwezo;wanakamati wawe na uwezo wa kusoma na kuandika kiswahili,na pia angalau wajue hesaba kidogo,ingawa kutojua hesabu haiwezi kuwa hoja kuu.
5)uwezo wa kujieleza ;wanakamati wawe na uwezo wenyeuwezo wa kujiuliza vizuri kwani,mara nyingi watapaswa kutembelea ofisi mbalimbali serikali katika kutafuta taarifa na nyaraka mbalimbali hivyo itabidi waweze kuelezea mahitaji yao.
                                KIMSINGI LAZIMA TUZINGATIE SANA KWANI KAZI HII TUNAFANYA NA WATU TOFAUTI KATIKA NYANJA TOFAUTI WANAKAMATI LAZIMA WAWE MAKINI SANA KATIKA HILI
                                      maswali ya na ruhusiwa unaweza tuma kupitia email pimal1990@gmail.com/0712064800
                                                             asante.

Thursday, 7 November 2013

MASUALA YA KUZINGATIA KABLA YA KUFANYA PETS KWA WANANCHI

1)unda kamati au kikundi cha PETS inayojumuisha makundi yote yakikiwemo wanawake na vijana
2)ainisha/bainisha secta husika kwa ajili ya ufatiliaji
3)bainisha namna ya kufatilia na kupata taarifa za kutosha kuhusu hali halisi ya sehemu husika kabla ya ufatiliaji
4)zingatia jinsi/namna ya kufanya ufatiliaji.
5)tambua wapi pa kwenda kwa ajili ya kupata taarifa husika
6)Nini au kitu gani cha kuuliza
7)nani wa kumuuliza
8)nini kifanyike kuhamasisha umma
9)jinsi ya kutoa mrejesho na kusambaza taarifa
10)hatua za kuchukua (ushawishi na utetezi)
11)kitu gani au nini kimebadilika?
12)vyanzo mbalimbali vya taarifa(TAKUKURU,TAMISEMI NK)

LAZIMA TUZINGATIE VITU MUHIMU KATIKA KUFANYA PETS KWANI INATURAHISISHIA KATIKA UFATILIAJI BILA KUVUNJA SHERIA ZA NCHI.
                 ombi langu vijana wezangu na watanzania kwa ujumla tujifunze mambo yaha yatatusaidia kwa faida yetu kama  kuna tatizo ujaelewa piga au tuma sms la swali lako utajibiwa 0712064800

















0

Wednesday, 30 October 2013

TANZANIA HATUNA VIONGOZI WAADILIFU.

Hisia zangu zinanituma kuandika maneno haya.
Ni wazi kabisa viongozi hapa nchini hawajui nini maana ya uadilifu au kama kama wanajua basi wanakusudia kufanya mambo yasiofaa katika jamii,sina maana ya viongozi wote si waadilifu ila penye asilimia nyingi basi tutasema karibia wote,waliokuwa waadilifu basi hawana nguvu ya kusema wala si raisi kujionyesha,UADILIFU ni neno pana sana na linaweza likawa soma kubwa sana ambalo viongozi wetu walitakiwa kupatiwa kabla hawajaanza kupokea madaraka kimsingi UADILIFU inajumuisha tabia zote ambazo zinampendeza binadamu katika kutenda haki na kumjali na kumuhurumia zaidi ya kujiurumia wewe mwenyewe,UADILIFU ni kufanya jambu zaidi bila kujali maslahi yako na ikiwezekana kuongeza zaidi ya uwezo wa kawaida ambao mtu si raisi kujitoa dhana hii inabeba tabia nyingi mfano lazima uwe na HEKIMA,BUSARA,UPOLE,UTARATIBU,MWENYE SIFA YA PEKEE,UPENDO,UKWELI,MWAJIBIKAJI KULIKO KAWAIDA,HURUMA na n.k hizi zote ni UADILIFU tunamifano ya watu duniani waliokuwa waadilifu kihistoria YESU CHRISTU,MTUME MOHAMAD na n.k,UADILIFU ni ile hari ya kujitolea kufanya jambo kwa ajili ya mtu mwingine bila kujali kitakacho kukuta ili kumpendeza MUNGU wako kulingana na imani.
Binafsi ningewaasa viongozi wa TANZANIA kujifunza UADILIFU ili kuweza kuifikisha mbali nchi yetu wajue kuurumia watoto,wamama,wazee,wa baba,vijana na hata walemavu ili siku moja wapate neema ya MUNGU.
                                asante.

Saturday, 26 October 2013

JE? TUNAWEZAJE KUUNDA KAMATI ZA UFATILIAJI WA RASILIMALI ZETU ?

Nashukuru sana  ndugu SALIMU KHAMISI kuuliza swali nzuri ila nitalijibu kwa faida ya watanzania wote.kamati hizi za PETS(ufatiliaji) zinzundwa na wananchi wanyewe iwe katika ngazi ya kijiji au mtaa,muhimu zaidi ni kuhakikisha kamati hii inaundwa na wahusika wa sehemu hiyo (wakazi),kila baada ya miezi mitatu serikali ya kijiji au mtaa mwenyekiti anawajibu wa kuitisha mkutano kuu ni lazima na mwana nchi hana haki ya kumuoji kiongozi wake kama mkutano ujafanyika,sasa katika mkutano huu hapo ndipo kamati hizo utengenezwa kwa kuchaguliwa na wananchi wenyewe kamati inatakiwa iwe na watu 7 hadi 15,muhimu kuachaguwa watu wenye sifa na kuhusisha jinsia yaani kila kundi lazima lishiriki,wanawake,wanaume,walemavu,vijana,na hata wazee.sifa muhimu asiwe nahitikadi za uchama(asitumie siasa katika kufanya kazi hii ya PETS)kushiriki kwa viongozi inategemeana na jinsi wananchi watakavyo hamua namaanisha kuwa kama kiongozi anaonekana ni msaada kwa jamii yake na wananchi wana mkubali anaweza akaingia kwenye kamati hizo.
                                kwa ufupi sana nimejibu ila ndugu watanzania tunaitaji elimu hii kwa ukalibu zaidi.
piga tena namba yangu upate maelekezo kama utakwama 0712064800 uliza maswali kwa faidi yetu sote

JE?UNAJUWA MUUNDO WA SERIKALI

Muhihimu sana kwa kila mtanzania kujuwa muundo wa serikali yetu,hii inaweza kutusaidia katika mchakato mzima wa ufatiliaji na kufikia malengo ya mwaka 2025 ya utawala bora,vijana wezangu,mama zangu,kaka zangu,na baba zangu bila kusahau wazee wangu lazima tutambue nchi ya Tanzania ni yetu na tunastahili kupata kile ambacho kinastahili kupata bila kuzulumiwa na mtu wowote.
MUUNDO WA SERIKLI upo katika mgawanyo wa serikali mbili ambazo ni SERIKALI KUU na SERIKALI ZA MITAA.serikali hizi uhundwa na wananchi wenyewe katika kuwachuguwa viongozi wao.tukianza na serikali kuu inahusisha viongozi wa ngazi za juu.serikali hii inamajukumu ya kusimamia majukumu ya utekelezaji wa sheria,kusimamia maslahi ya wananchi,kutoa ulinzi na usalama,kuwapa wananchi huduma stahili kama afya,elimu,ujenziwa miundo mbinu,n.k haya yote ni majukumu ya serikali.serikali kuu inaviongozi wake TAASISI YA URAHISI,MAKAMU WA RAHISI,WAZIRI MKUU ambae ni kiongozi na msimamizi wa shughuli zote.
SERIKALI ZA MITAA inaundwa na mamlaka ya mji,manispaa ya mji,na mamlaka ya vijiji ambayo inajumuhisha halmashauri ya wilaya..hizi serikali mbili zinahusiana katika majukumu ya kazi mfano serikali kuu utekeleza majukumu yake kwa kufanya ugatuzi wa madaraka katika serikali za mitaa.
(kwa kuwa watanzania hatuna desturi ya kusoma basi niishie hapo kama utakuwa na swali uliza kupitia namba 0712064800 utapata jibu hapo hapo)
                     asante mafunzo haya natoa bure kwa mtazania yoyote yule ili tubadilishe taifa letu.

Friday, 25 October 2013

MAFUNZO YA PETS BURE

PETS(PUBLIC EXPENDICTURE TRACKING SYSTEM OR SURVEY)mfumo wa ufatiliaji wa matumizi wa rasilimali za umma,.
Huu ni mfumo rafiki ambao unawaitaji viongozi wetu kuwa wawajibikaji na wawazi na kuwa na usawa katika jamii ya kitanzania.Hivyo basi mfumo huu upo sambamba kabisa na mapato na matumizi katika muundo mzima wa serikali.Jambo la msingi ni kujua kodi zetu ndo zinaleta maendeleo katika nchi yetu hivyo wananchi tunahaki ya kuoji na kuuliza na kukemea pale unapotokea ubadhirifu hivyo tutambue kuwa watu wote wa serikali tunawalipa sisi wananchi kwa kodi zetu hivyo tusikubali kodi zetu zitumike vibaya pasipo na sababu ya msingi tena kwa faida ya mtu binafsi ila tudai haki ya kodi zetu kwa kufanya shughuri za kimaendeleo zaidikuliko za kawaida.mfano unakuta viongozi wanapanga bajeti kubwa katika matumizi ya kawaida kuliko ya maendeleo.LAZIMA WATANZANIA IFIKE WAKATI TUFATILIE MATUMIZI YA FEDHA ZETU AMBAZO NI KODI KILA MWANANCHI ANALIPA KODI JE?SERIKALI INAWAJIBIKA KATIKA PESA ZETU?.naitwa mwezeshaji JOSEPH MALISA natoa mafunzo haya bure kabisa katika kamati yoyote hapa nchi.gharama ya nauli juu yenu namba zangu 0712064800