Translate

Translate

Saturday, 18 April 2015

BARABARA ZA JAZWA VIFUSI VYA MATOPE MTAA WA MAKANGARAWE WILAYA YA TEMEKE


 Juhudi za maendeleo mtaa wa Makangarawe Wilaya ya Temeke Jijini Dar es salaam Serikali imejaza vifusi  barabara za mtaa wa Makangarawe jinsi ambavyo wananchi wa maeneo hayo wakilalamika kuwa vifusi hivyo ni matope matupu kipindi cha mvua zikianza kunyesha.

Juhudi hizo za serikali ziliongozwa na mwenyekiti wa mtaa kuhakikisha zoezi ilo linakamilika.





Hitambulike kuwa fedha zinazotumika katika ujenzi huu ni fedha za  wananchi hivyo kuweka vifusi ambavyo vinaongeza gharama ni ufujaji wa fedha za umma pasipo malengo, Ni wazi kabisa uwekaji huu wa vifusi ni wakibabaishaji ambao matokeo yake ni matumizi mabaya ya fedha.

Wananchi wanahaki wa kukemea jambo kama ili na kuligomea ili kuonesha msimamo wao ili mambo kama haya ya matumizi mabaya ya fedha yasijitokeze kama serikali inaamuwa kuweka vifusi barabara za mtaa basi hihakikishe inaweka kifusi cha uhakika na cha kudumu chenye mwendelezo kuliko kuweka matope ambayo na chafuzi katika mazingira yetu

Wananchi inawapasa watambue MATUMIZI MABAYA NI UBADHILIFU hivyo vipigwe vita tabia hii.








WANAFUNZI HATARINI NA MAGONJWA YA MRIPUKO SHULENI

Ni katika hari ya kutisha sana ambayo mwandishi amethibitisha hatari iyo ambayo inapelekea magonjwa ya mripuko kama kipindupindu hata magonjwa ambayo yataendana na mazingira machafu pasipo kutuzwa . Hari hii imejionesha katika baadhi ya shule za wilaya ya Temeke jijini  Dar es salaam jambo ambalo ni hatari sana kwa afya za watoto ambao wapo shuleni .


 serikali na wananchi 
inabidi kushirikiana ili kuweza kuhakikisha mazingira salama na yenye kuleta afya bora sehemu zote zinazohitaji huangalizi ili kuhepusha baraa la magonjwa ya mripuko mashuleni
 ASANTE

Friday, 13 February 2015

MRADI WA MAJI SAFI MAKANGARAWE NI TATIZO KWA WANANCHI

Tatizo la Maji safi Mtaa wa Makangarawe, katika Kata ya Makangarawe Wilaya ya Temeke jiji Dar es salaam umezidi kuwa ni shida kwa wananchi, jambo ambalo linapelekea wananchi wengi kutumia visima vya watu binafsi ambavyo usalama wa maji si mzuri kiafya .


Akizungumza kwenye mkutano wa wananchi mwenyekiti wa sasa Ndugu Juma Mohamed Kibanda juu ya tatizo la mradi huo kufika huko alisema”hii inatokana na usimamizi mbovu wa uongozi uliopita madarakani ,uongozi kukosa uwazi na uwajibikaji jambo ambalo limepelekea mradi huu wa maji safi na salama kufa na wananchi wetu kuangaika”
Baadhi ya mfumo wa mabomba ya maji yamepasuka kusabisha maji mengi kuvuja na kusambaa maeneo mbalimbali ya mtaa, na kusababisha uchafuzi wa mazingira katika maeneo hayo ambapo ni hatari kwa afya ya jamii iliyo zunguka maeneo hayo.
Uongozi utambue wananchi wako katika mazingira hatarishi ya kiafya na hata upatikanaji wa maji safi na salama hivyo iwe ni changamoto kwao ili kutafuta ufumbuzi wa tija kuondoa tabu hiyo.



Na; Joseph malisa 

Wednesday, 11 February 2015

TASAF MTAA WA MAKANGARAWE TEMEKE WAZUA MASWALI MENGI

TASAF MTAA WA MAKANGARAWE TEMEKE WAZUA MASWALI MENGI
Mpango wa serikali wa kunusuru kaya maskini awamu ya tatu (TASAF) ukiwa katika utekelezaji wake wa kuhakikisha wanawafikia walengwa wa mradi huo ambao kaya maskini umepelekea kuwemo kwa maswali mengi ya msingi  kutoka kwa baadhi ya wananchi walio hudhuria kikao hicho mtaa Makangarawe,Kata ya Makangarawe, Wilaya Temeke Dar es salaam.



Akizungumza katika mkutano   mwenyekiti wa mtaa Juma Mohamed Kibanda alisema"Mpango huu wa TASAF ni mpango wa kunusuru kaya maskini ambao kwa sasa umetufika wanamakangarawe hivyo tushirikiane katika kufikia lengo na kuwafikia walengwa"aliendelea kusema "Mpango huu ni wamendeleo hasa katika kaya maskini ". Akizungumza  mwezeshaji wa TASAF ambae alielezea malengo na faida za mpango huo wa TASAF. Jambo ambalo lilizua maswali mengi na hoja za msingi kutoka kwa wanajamii wa Makangarawe  ili kujilidhisha kama mpango huo ni waukweli au ni jambo la kisiasa ambalo linaleta mkanganyiko kutokana na ukaribu wa uchaguzi jambo ambalo lishawahi kujitokeza mwaka 2005 .
Kufatiwa mkutano huo mwenyekiti Juma Kibanda aliwasihi hasa vijana wajitambue na waitambue serikali yao hasa katika maswala ya kimaendeleo na kuleta mabadiliko katika mtaa wao.


Wednesday, 7 January 2015

MAMBO KUMI NA MOJA YA KUZINGATIA KABLA YA KUFANYA PETS (VIEW BLOG)

UTARATIBU WA WANANCHI KUENDESHA PETS
MASUALA YA KUZINGATIA KABLA YA KUFANYA PETS
·      Unda kamati au kikundi cha PETS inayojumuisha uwakilishi wa makundi yote wakiwemo wanawake na vijana.
·      Ainisha/bainisha sekta husika kwa ajili ya ufatiliaji
·      Bainisha namna ya kufuatilia na kupata taarifa za kutosha kuhusu hali halisi ya sehemu husika kabla ua ufatiliaji
·      Zingatia jinsi/namna ya kufanya ufuatiliaji
·      Tambua wapi pa kwenda kwa ajili ya kupata taarifa husika
·      Nini / kitu gani cha kuuliza
·      Nini kifanyike kuhamasisha umma
·      Jinsi ya kutoa mrejesho na kusambaza taarifa
·      Hatua za kuchukua (ushawishi na utetezi)
·      Kitu gani au nini kimebadilika?

·      Vyanzo mbalimbali vya taarifa (TAKUKURU, TAMISEMI nk)

Tuesday, 6 January 2015

MALENGO YA UFUATILIAJI- PETS

PETS imethibitika kuwa ni kati ya zana na nyenzo muhimu katika ufuatiliaji wa matumizi ya rasilimali za umma , hasa pale inapofanyika kwa mitizamo wa kijinsia . Hivyo basi , PETS inalenga kufanikisha yafuatayo;

Ø Kuboresha utoaji huduma ; kufuatilia matumizi ya fedha au rasilimali za umma kwa mtizamo wa kijinsia , kunasaidia sana kuchochea uboreshaji wa utoaji wa huduma mbalimbali za kijamii kwa ubora uliokusudiwa . vile vile kuhakikisha kuwa rasilimali zimeenda kutekeleza lengo kusudiwa na kuhakiki thamani halisi ya fedha zilizotumika.
Ø Kuhakiki utendaji wa serikali na mamlaka husika; mfumo huu unasaidia sana katika kuhakiki utendaji wa serikali na mamlaka husika ,hasa katika ngazi za vitongoji na vijiji au katika vikundi vidogo vidogo , kwa kusoma nyaraka , ripoti na taarifa mbalimbali za utekelezaji.
Ø Kukuza uwajibikaji;  Hii inaanzia kwa wananchi kwa maana ya wanawake , wanaume , vijana , walemavu na makundi mengine yaliyoko pembezoni , ambapo hushiriki moja kwa moja katika kuhoji serikali .sanjali na hilo huhakikisha kwamba viongozi wanatenda kila ambacho wanapaswa kutenda kulingana na mipango.
Ø Kuwezesha uandaaji wa mipango shirikishi ya maendeleo;  Taarifa zinawafanya wananchi waweze kushiriki vizuri katika uandaaji wa mipango ,au katika kubaini aina ya miradi itakayotekelezwa kwenye jamii hisika


Friday, 2 January 2015

JE? TANZANIA INA UTAWALA BORA click usome kujua nini utawala bora

UTAWALA BORA
Utawala bora ni matumizi ya uwezo (mamlaka)wa kiserikali katika jitihada za kuongeza na kutumia rasilimali hizo ili kuboresha maisha ya wananchi
MISINGI YA UTAWALA BORA
v      Utawala wa kidemokrasia
v      Ushirikishwaji wa umma
v      Utawala wa kisheria
v      Haki na usawa kwa watu wote
v      Uwazi katika kuendesha shughuli za maendeleo
v      Uwajibikaji katika utendaji
v      Uadilifu
Misingi hii ikizingatiwa na kufanyiwa utekelezaji lazima mabadiliko yataonekana

Ili utawala bora uwe na sifa za kupendeza na kuendwa na wananchi lazima uzingatie Misingi ya utawala bora.

TEC MEDIA vs YOUTHCAN VIDEO

SOMA UFAHAMU KWA KINA JUU YA KAMATI ZA SERIKALI ZINAVYOKWENDA KINYUME NA SHERIA ZA NCHI kwa faida yetu sote

KAMATI  ZA HALMASHAURI YA KIJIJI/KAMATI YA MTAA

Ø Kuna kamati tatu za halmashauri ya kijiji/mtaa kisheria
Ø Kamati ya fedha,mipango na uchumi ,huduma za jamii na shughuli za kujitegemea na ulinzi na usalama
Ø Mkutano mkuu wa kijiji/mkutano wa wakazi wa mtaa una uwezo wa kuagiza halmashauri ya kijij/kamati ya mtaa kuundaa kamati ya muda kwa shughuli maalum au halmashauri yenyewe inaweza kuunda kukiwa na haja ya kufanya hivyo.
Ø Idadi ya wajumbe katika kamati inashauriwa wasipungue wajumbe watatu 3 na wasizidi wajumbe watano 5
Ø Kamati za kisheria inafaa ziongozwe na mjumbe wa halmashauri ya kijiji /kamati y mtaa
Ø Inashauriwa wenyekiti wa kijiji /mtaa , wenyeviti wa vitongoji  wasiwe wenyeviti wa kamati mbalimbali ili kutolimbikiza madaraka yote kwa halmashauri ya kijiji/kamati ya mtaa
Ø Wananchi  wakaida wanaweza kuwa wajumbe wa kamati au wanaweza kuitwa kutoa ushauri kwenye vikao vya kamati
Ø  Kamati zinaweza kukutana mara kwa mara kutunza kumbukumbu na kuendesha vikao kwa kushauriwa na afisa mtendaji wa kijiji (VEO)/ Afisa mtendaji wa mtaa(MEO)

Thursday, 1 January 2015

JE? WAJUA WAJIBU WETU KWENYE SERIKALI ZA MTAA/KIJIJI? soma kwa utulivu utagundua mapungufu yetu na ya serikali usika

Mwananchi ana wajibu na majukumu yake kuhakikisha kuwa kiongozi aliyemchagua au kuteuliwa anatimiza wajibu wake ipasavyo katika viwango vinavyokubalika katika eneo la kijiji/mtaa kulingana na mipango na makibaliano ya vikao vya kisheria ya kijij na mtaa.
Kila mwananchi ana wajibu wa kupinga na kukataa kila aina ya uovu kayika jamii ikiwemo rushwa,uonevu wizi ubadhilifu wa mali za umma nay a watu binafsi.

Wananchi pia wana jukumu la kudai na kupigania haki zao na za wananchi wengine kutoa malalamiko na kuuliza maswali juu ya mambo mbalimbali yananoendelea kijijini au kwenye mtaa kupitia vyombo mbalimbali vya kijamii na kiserikali. Wananchi wanashiriki katika serikali za mitaaa kupitia vikao au mikutano mbalimbali ambapo hujadili na kutoa mapendekezo  yao kuhusu mipango na matatizo yanayowakabili kwa mamna moja au nyingine ili kuweza kupatiwa ufumbuzi na kurahisisha uboreshaji wa huduma za kijamii katika maeneo yao wanamoishi.